NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 25

Somo la 25

Ingia chini ya dawati.

Anna amehudhuria darasa la somo la Kijapani na jengo la shule likaanza kutikisika.

Somo la 25 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

TSUKUE NO SHITA NI HAIRE

Mazungumzo

先生 地震だ。みんな、落ち着いて。
机の下に入れ。
Ni tetemeko. Nyote, muwe watulivu. Ingia chini ya dawati.
Mwalimu JISHIN DA. MINNA, OCHITSUITE.
TSUKUE NO SHITA NI HAIRE.
Ni tetemeko. Nyote, muwe watulivu. Ingia chini ya dawati.
先生 揺れは収まったようだ。 Inaonekana mitetemo imetulia.
Mwalimu YURE WA OSAMATTA YÔ DA.
Inaonekana mitetemo imetulia.
アンナ びっくりした。日本は本当に地震が多いですね。 Nilishangazwa. Kwa kweli Japani hushuhudia mitetemo mingi, au siyo?
Anna BIKKURI SHITA. NIHON WA HONTÔ NI JISHIN GA ÔI DESU NE.
Nilishangazwa. Kwa kweli Japani hushuhudia mitetemo mingi, au siyo?

Vidokezo vya sarufi

YÔ DA / YÔ DESU

YÔ DA ni namna ya kawaida ya YÔ DESU, inayoonyesha kwamba mzungumzaji ametathmini hali ilivyo na kufanya maamuzi fulani kuhusiana na hali hiyo.
Kabla ya YÔ DA, huwezi kutumia vitenzi vya umbo la MASU.
k.m.) YURE WA OSAMATTA YÔ DA.
(Inaonekana mitetemio imekwisha.)

* OSAMATTA = Umbo la TA la OSAMARIMASU (kutulia)

Tofauti kati ya WA na GA

WA: inaonyesha mada
GA:  inaonyesha kiima

WA inaonyesha mada ya sentensi. Na kiima kina uhusiano na mada, na kinaonyeshwa na GA na wakati mwingine WA.

k.m.) ZÔ WA HANA GA NAGAI.
(Kuhusu ndovu, mikonga yao ni mirefu.)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la amri la vitenzi
Hivi ndiyo jinsi ya kutengeneza umbo la amri kutoka kitenzi cha umbo la MASU. Kwanza, kwa vitenzi vinavyomalizia na irabu "E" kwenye silabi kabla tu ya MASU, unabadilisha MASU na kuwa RO. Kwa mfano, “kula,” TABEMASU, inabadilika na kuwa TABERO, (Kula!).

Tanakali Sauti

Kutikisika
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Tetemeko la ardhi linapotokea, kitu cha kwanza unachohitajika kufanya ni kupata taarifa kupitia redio au runinga. Niliambiwa nifanye hivyo.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.