NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Maswali yanayojirudia na majibu yake

Maswali yanayojirudia na majibu yake

Q.1 Nawezaje kupakua maandiko ya "Jifunze Kijapani"?

A.1

Ingia katika ukurasa wa kupakua. Fuata maelekezo katika ukurasa huo ili kupakua maandiko. Unaweza pia kupakua maandiko kutoka katika ukurasa wa masomo.

Funga ×

Q.2 Ni aina gani ya masomo na vifaa vya kusomea vinavyopatikana kwenye tovuti?

A.2

Kuna masomo 48 ambayo unaweza kuyatumia kujifunza misemo mbalimbali kupitia mazungumzo. Zaidi ya hayo, kuna Herufi za Kijapani, Majaribio ya misamiati, Maelezo ya sarufi kutoka kwa mtaalam wa Kijapani na utambulisho wa Tanakali sauti.

Funga ×

Q.3 Siwezi kusikiliza kipindi cha "Jifunze Kijapani" kwenye tovuti kwa sababu ya mazingira mabaya ya mtandao.

A.3

"Jifunze Kijapani" inatangazwa kama kipindi cha NHK WORLD RADIO JAPAN. Tafadhali bofya hapa ili ufahamu kuhusu muda na masafa.

Funga ×

Q.4 Kuna kitu sielewi kuhusu Kijapani. Je, mtawasiliana nami iwapo nitauliza swali kupitia barua pepe?

A.4

"Jifunze Kijapani" hakina huduma za kujibu maswali ya watu binafsi kupitia barua pepe au barua. Maswali yenu tutayajibu kupitia kipindi cha NHK WORLD RADIO JAPAN au kupitia tovuti hii. Tafadhali tumia fomu ya barua pepe kututumia swali lako.

Funga ×

Q.5 Je, kuna vipindi vya redio au tovuti ambapo naweza kupitia tena masomo yaliyopita na kufanya majaribio ya uwezo wangu wa lugha ya Kijapani?

A.5

Kuna kipindi cha "Mapitio: Lipi Sahihi?" katika redio na tovuti. Kipengele hicho kinakupa fursa ya kupitia tena masomo katika mfumo wa majaribio. Kwenye tovuti yetu pia kuna "Orodha ya misamiati na Majaribio", ambapo unaweza kupitia tena misemo inayojitokeza kwenye masomo.

Funga ×

Q.6 Je, kuna programu yoyote ya "Jifunze Kijapani"?

A.6

Hatuna programu maalum ya "Jifunze Kijapani" kwa ajili ya simu za smartphones. Hata hivyo, kuna programu ya NHK WORLD RADIO JAPAN ambayo inakuwezesha kusikiliza masomo ya hivi karibuni.

Funga ×

Q.7 Ningependa kuwa na rafiki wa Japani wa kuwasiliana naye. Mnaweza kunitambulisha kwa yeyote?

A.7

Samahani, huduma hiyo haitolewi na NHK WORLD.

Funga ×

Q.8 Je, mnatoa vyeti kuthibitisha kuwa nimekamilisha masomo ya "Jifunze Kijapani"?

A.8

Hapana, hatutoi vyeti vya aina yoyote kwa masomo ya "Jifunze Kijapani".

Funga ×