NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 18

Somo la 18

Nimepotea njia.

Anna alitembelea duka la kuuza vitabu pamoja na rafiki zake, Sakura na Rodrigo. Baada ya kuondoka kwenye duka hilo, Anna alipoteleana na wenzake.

Somo la 18 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

MICHI NI MAYOTTE SHIMAIMASHITA

Mazungumzo

アンナ もしもし、さくらさん。助けてください。
道に迷ってしまいました。
Halo, Sakura. Tafadhali nisaidie. Nimepotea njia.
Anna MOSHIMOSHI, SAKURA-SAN. TASUKETE KUDASAI.
MICHI NI MAYOTTE SHIMAIMASHITA.
Halo, Sakura. Tafadhali nisaidie. Nimepotea njia.
さくら 今、どこ? Uko wapi hivi sasa?
Sakura IMA, DOKO?
Uko wapi hivi sasa?
アンナ 目の前に郵便局があります。 Mbele yangu kuna ofisi ya posta.
Anna ME NO MAE NI YÛBINKYOKU GA ARIMASU.
Mbele yangu kuna ofisi ya posta.
さくら 分かった。そこにいて。 Nimeelewa. Baki hapo ulipo.
Sakura WAKATTA. SOKO NI ITE.
Nimeelewa. Baki hapo ulipo.

Vidokezo vya sarufi

Kitenzi cha umbo la TE + SHIMAIMASHITA

Unasema SHIMAIMASHITA baada ya kitenzi cha umbo la TE ili kuonyesha umefanya jambo bila uangalifu au unajutia ulichokifanya.

k.m.)
MACHIGAEMASU (kukosea)
>>  MACHIGAETE SHIMAIMASHITA (Nimekosea)

Ili kujifunza zaidi, tafadhali soma "Mwalimu, Tufundishe."

Mwalimu Tufundishe

Kitenzi cha umbo la TE + SHIMAIMASHITA
Ukisema SHIMAIMASHITA baada ya kitenzi cha umbo la TE, unasema ya kwamba umemaliza au umekamilisha jambo ulilokuwa ukifanya, na huwezi kulirejesha katika hali yake ya awali. Kwa hiyo mara nyingi unatumia SHIMAIMASHITA, ikiwa umekosea kufanya jambo fulani na unajutia.

Tanakali Sauti

Kuchanganyikiwa / kuzunguka bila kujua cha kufanya
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Niliambiwa ikiwa nimepotea njia, ninaweza kwenda kwenye kituo cha polisi. Afisa wa polisi ataniambia muelekeo kwa kunionyesha ramani.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.