Somo la 17
Pendekezo lako ni lipi?
Kwenye duka la vitabu, Anna ameona vitabu vingi vya manga ambavyo vinaonekana kumvutia. Hawezi kuamua ni kipi atakachokinunua.
Usemi wa msingi:
OSUSUME WA NAN DESU KA
Mazungumzo
アンナ | あ、この本いいなあ。あれも面白そう。 | Ah! Kitabu hiki ni kizuri. Kile pia kinaonekana kuvutia.
|
---|---|---|
Anna | A, KONO HON II NÂ. ARE MO OMOSHIROSÔ.
Ah! Kitabu hiki ni kizuri. Kile pia kinaonekana kuvutia.
|
|
アンナ | さくらさんのおすすめは何ですか。 | Sakura, pendekezo lako ni lipi?
|
Anna | SAKURA-SAN NO OSUSUME WA NAN DESU KA.
Sakura, pendekezo lako ni lipi?
|
|
さくら | これはどう? | Unaonaje kuhusu hiki?
|
Sakura | KORE WA DÔ?
Unaonaje kuhusu hiki?
|
|
アンナ | ホラーはちょっと…。 | Simulizi za kutisha kidogo mimi aah....
|
Anna | HORÂ WA CHOTTO....
Simulizi za kutisha kidogo mimi aah....
|
Vidokezo vya sarufi
WA CHOTTO
Unaweza kusema hivi kukataa pendekezo kwa namna ya kiungwana, ama isiyo ya moja kwa moja.
k.m.) HORÂ WA CHOTTO.... (Simulizi za kutisha mimi kidogo aah....)
Tanakali Sauti
Ukimya / Kujipanga kwenye mstari
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Duka kubwa la vitabu lina tarakilishi za kutafutia vitabu kwa ajili ya wateja. Tunaweza kuzitumia kutafuta ikiwa duka husika lina kitabu fulani unachotafuta na wapi kilipo.
Ni jambo linalorahisisha mchakato wa utafutaji vitabu.