NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Maswali yanayojirudia na majibu yake

Maswali yanayojirudia na majibu yake

Q.1 Ninawezaje kupakua sauti, maandishi na picha za "Jifunze Kijapani"?

A.1

Nenda kwenye ukurasa wa kupakua. Fuata maagizo yaliyopo kwenye ukurasa huo ili uweze kupakua sauti na maandishi ambayo pia yanaweza kupakuliwa kutoka kwenye ukurasa ulio na masomo. Huduma ya podcast kwa ajili ya sauti pia inapatikana.
Huwezi kupakua picha. Tafadhali ifurahie kwenye tovuti.

Funga ×

Q.2 Ni aina gani ya masomo na vifaa vya kusomea vinavyopatikana kwenye tovuti?

A.2

Kuna masomo 48 ambayo unaweza kuyatumia kujifunza misemo mbalimbali kupitia mazungumzo. Zaidi ya hayo, kuna Herufi za Kijapani, Majaribio ya misamiati, Maelezo ya sarufi kutoka kwa mtaalam wa Kijapani na utambulisho wa Tanakali sauti.

Funga ×

Q.3 Siwezi kusikiliza kipindi cha "Jifunze Kijapani" kwenye tovuti kwa sababu ya mazingira mabaya ya mtandao.

A.3

"Jifunze Kijapani" inatangazwa kama kipindi cha NHK WORLD RADIO JAPAN. Tafadhali bofya hapa ili ufahamu kuhusu muda na masafa.

Funga ×

Q.4 Kuna kitu sielewi kuhusu Kijapani. Je, mtawasiliana nami iwapo nitauliza swali kupitia barua pepe?

A.4

"Jifunze Kijapani" hakina huduma za kujibu maswali ya watu binafsi kupitia barua pepe au barua. Maswali yenu tutayajibu kupitia kipindi cha NHK WORLD RADIO JAPAN au kupitia tovuti hii. Tafadhali tumia fomu ya barua pepe kututumia swali lako.

Funga ×

Q.5 Siwezi kucheza sauti kutoka kwenye ukurasa wa masomo.

A.5

Baadhi ya simu za Smartphone na tarakirishi ya kiganjani zinaweza kushindwa kucheza sauti kutoka kwenye ukurasa wa masomo. Katika matukio kama hayo, tafadhali fuata hatua zifuatazo ili uweze kupakua sauti.

  1. Pakua sauti ya masomo kutoka kwenye ukurasa wa kupakulia au katika ukurasa wa kila somo. Namna ya kupakua inaweza kupatikana upande wa juu wa sehemu hii ya maswali yanayojirudia na majibu yake.
  2. Ukishapakua bila matatizo yoyote, tumia programu ya kucheza muziki iliyopo kwenye kitumi chako kuchezesha sauti.
  3. Tafadhali fungua mtandao huku ukiendelea kuchezesha sauti ya somo ulilolipakua chini kwa chini.

Funga ×

Q.6 Ningependa kupata CD ya "Jifunze Kijapani". Je, ninaweza kuinunua kwa njia ya Posta?

A.6

"Jifunze Kijapani" hakijahifadhiwa kwenye CD. Tafadhali pakua faili ya sauti iliyopo kwenye tovuti hii. Unaweza kupakua bila malipo yoyote.

Funga ×

Q.7 Je, ninaweza kupakua mifululizo iliyopita ya masomo ya "Jifunze Kijapani" katika mfumo wa sauti na maandishi, na wahusika kama Cuon na Leo?

A.7

Hatutoi huduma ya kupakua sauti na maandishi ya mifululizo iliyopita ya "Jifunze Kijapani".

Funga ×

Q.8 Je, kuna vipindi vya redio au tovuti ambapo naweza kupitia tena masomo yaliyopita na kufanya majaribio ya uwezo wangu wa lugha ya Kijapani?

A.8

Kuna kipindi cha "Mapitio: Lipi Sahihi?" katika redio na tovuti. Kipengele hicho kinakupa fursa ya kupitia tena masomo katika mfumo wa majaribio. Kwenye tovuti yetu pia kuna "Orodha ya misamiati na Majaribio", ambapo unaweza kupitia tena misemo inayojitokeza kwenye masomo.

Funga ×

Q.9 Ninawezaje kupata kitabu cha "Jifunze Kijapani?"

A.9

Tutatuma kitabu kwa njia ya posta mara baada ya kupokea maombi. Lakini huduma hii inapatikana kwa wasilizaji wa kipindi cha "Jifunze Kijapani" nje ya Japani, na si wale wanaotumia tovuti ya Jifunze Kijapani. Ikiwa unataka nakala ya kitabu hicho, tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia fomu hii. Ikiwa huwezi kutumia fomu, wasiliana nasi kwa njia ya posta. Unapowasiliana nasi, tafadhali andika jina lako, anuani na maoni kuhusu "Jifunze Kijapani".

Funga ×

Q.10 Je, kuna programu yoyote ya "Jifunze Kijapani"?

A.10

Hatuna programu maalum ya "Jifunze Kijapani" kwa ajili ya simu za smartphones. Hata hivyo, kuna programu ya NHK WORLD RADIO JAPAN ambayo inakuwezesha kusikiliza masomo ya hivi karibuni.

Funga ×

Q.11 Ningependa kuwa na rafiki wa Japani wa kuwasiliana naye. Mnaweza kunitambulisha kwa yeyote?

A.11

Samahani, huduma hiyo haitolewi na NHK WORLD.

Funga ×

Q.12 Je, mnatoa mafunzo ya maandishi ya kanji?

A.12

Hapana, hatutoi mafunzo ya maandishi ya kanji.

Funga ×

Q.13 Je, mnatoa mafunzo ya muendelezo na ya juu ya "Jifunze Kijapani"?

A.13

Hapana, hatutoi huduma hiyo.

Funga ×

Q.14 Je, mnatoa vyeti kuthibitisha kuwa nimekamilisha masomo ya "Jifunze Kijapani"?

A.14

Hapana, hatutoi vyeti vya aina yoyote kwa masomo ya "Jifunze Kijapani".

Funga ×