NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 32

Somo la 32

Napenda zaidi futoni.

Anna atalala katika nyumba ya bibi yake Sakura. Hii ni mara yake ya kwanza kulala kwenye futoni, ambalo ni godoro la kijapani na matandiko yake.

Somo la 32 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

FUTON NO HÔ GA SUKI DESU

Mazungumzo

さくら 布団とベッドとどちらが好き? Unapenda kulala kwenye futoni au kitandani?
Sakura FUTON TO BEDDO TO DOCHIRA GA SUKI?
Unapenda kulala kwenye futoni au kitandani?
アンナ 布団のほうが好きです。
この布団はベッドよりやわらかいです。
Napenda zaidi futoni.
Futoni hili ni laini kuliko godoro linalowekwa kitandani.
Anna FUTON NO HÔ GA SUKI DESU.
KONO FUTON WA BEDDO YORI YAWARAKAI DESU.
Napenda zaidi futoni. Futoni hili ni laini kuliko godoro linalowekwa kitandani.
アンナ それじゃ、おやすみなさい。 Basi, usiku mwema.
Anna SOREJA, OYASUMINASAI.
Basi, usiku mwema.
さくら おやすみ。 Nawe pia usiku mwema.
Sakura OYASUMI.
Nawe pia usiku mwema.

Vidokezo vya sarufi

A TO B TO DOCHIRA GA Kivumishi DESU KA

Unapomtaka mtu alinganishe sifa za A na zile za B, unasema  A TO B TO DOCHIRA GA  na baada ya hapo unataja kivumishi kikifuatiwa na DESU KA.

k.m.)
FUTON TO BEDDO TO DOCHIRA GA SUKI DESU KA. (Unapenda kulala kwenye futoni au kitandani?)

Mwalimu Tufundishe

Kauli ya kulinganisha kwa kutumia NO HÔ GA na YORI
Vivumishi vya Kijapani havina mnyambuliko wa ulinganifu. Kwa hiyo, unaelezea ulinganifu kwa kutumia YORI (kuliko), na NO HÔ GA (zaidi).

Tanakali Sauti

Ulaini
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kwa mara ya kwanza nimelala kwenye futoni. Bibi alikuwa amelianika juani kwa ajili yangu. Kwa hiyo, lilikuwa FUKA FUKA na lenye starehe.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.