NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 31

Somo la 31

Tayari nina umri wa miaka 82.

Anna ametembelea nyumbani kwa bibi yake Sakura, jijini Shizuoka. Bibi anaishi peke yake, na anatunza shamba dogo.

Somo la 31 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

MÔ HACHIJÛNI SAI DESU YO

Mazungumzo

アンナ おばあさん、お元気ですね。 Bibi, bado una nguvu na afya, au siyo?
Anna OBÂSAN, OGENKI DESU NE.
Bibi, bado una nguvu na afya, au siyo?
おばあさん もう82歳ですよ。
さあ、お茶をどうぞ。
Tayari nina umri wa miaka 82.
Tafadhali, karibu chai.
Bibi MÔ HACHIJÛNI SAI DESU YO.
SÂ, OCHA O DÔZO.
Tayari nina umri wa miaka 82. Tafadhali, karibu chai.
アンナ わあ、きれいな緑色。香りもいいです。 Oh! Ina rangi ya kijani ya kupendeza. Ina harufu nzuri pia.
Anna WÂ, KIREINA MIDORI IRO. KAORI MO II DESU.
Oh! Ina rangi ya kijani ya kupendeza. Ina harufu nzuri pia.

Vidokezo vya sarufi

Namba (2)

Tujifunze namba za takwimu mbili.
Tafadhali nenda kwenye "Nyenzo za kujifunzia."

Mwalimu Tufundishe

O na GO zinazoonyesha heshima
Unapotaka kuonyesha heshima kwa msikilizaji au mtu unayemzungumzia, unasema O au GO kabla ya nomino au vivumishi kuhusiana na mtu huyo. Kwa mfano, SHIGOTO (kazi) inakuwa OSHIGOTO. GENKI (kuwa na afya) inakuwa OGENKI. Na KAZOKU (familia) inakuwa GOKAZOKU.

Tanakali Sauti

Kunywa
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Chai iliyotayarishwa na bibi ilikuwa nzuri! Nimeanza kupata ladha ya chai ya kijani isiyokuwa na sukari.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.