NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Herufi HA inapotamkwa kama WA (Somo la 6)

Mwalimu Tufundishe

Herufi HA inapotamkwa kama WA (Somo la 6)

Katika siku za nyuma, WA inayoonyesha mada ilitamkwa na kuandikwa kama HA. Matamshi yake yamebadilika polepole na kuwa WA, lakini bado inaandikwa kama HA. Utaratibu huo unaweza kuwa vivyo hivyo kwa WA kwenye neno la KONNICHIWA (habari za mchana?). Inatamkwa kama WA, lakini inaandikwa kama HA. Mwanzoni, neno hili lilijumuisha neno linalomaanisha “leo” na HA iinayoonyesha mada. Ilikuwa ikitumiwa kumsemesha mtu katika mazungumzo ya kawaida. Kwa sasa, KONNICHIWA ni salamu ya kawaida inayotamkwa kama neno moja.

Kwenye sentensi ya DENWA O SHIMASU (Nitakupigia), O inayoonyesha mtendwa ilitamkwa katika namna tofauti miaka iliyotangulia. Kwa sasa, inatamkwa kama O. Lakini kwa kuandika bado inatumika herufi ya matamshi ya zamani.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.