Somo la 45
Kheri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa!
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Anna. Rafiki zake wanasherehekea siku hiyo mgahawani.
Usemi wa msingi:
OTANJÔBI OMEDETÔ
Mazungumzo
みんな | アンナ、お誕生日おめでとう。 | Anna, heri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa!
|
---|---|---|
Wote | ANNA, OTANJÔBI OMEDETÔ.
Anna, heri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa!
|
|
健太 | これ、ほんの気持ちです。 | Hiki ni kitu kidogo kwa ajili yako.
|
Kenta | KORE, HONNO KIMOCHI DESU.
Hiki ni kitu kidogo kwa ajili yako.
|
|
アンナ | どうもありがとうございます。 | Nakushukuru sana.
|
Anna | DÔMO ARIGATÔ GOZAIMASU.
Nakushukuru sana.
|
|
さくら | 何をもらったの? | Umepewa nini?
|
Sakura | NANI O MORATTA NO?
Umepewa nini?
|
|
アンナ | 開けてもいいですか。 | Ninaweza kufungua?
|
Anna | AKETE MO II DESU KA.
Ninaweza kufungua?
|
Vidokezo vya sarufi
MORAIMASU
Ikiwa mpokeaji ndiye kiima, unatumia MORAIMASU (kupewa/kupokea). Tumia NI, kuonyesha mtoaji.
k.m.) KANOJO WA KARE NI FÛSEN O MORAIMASU.
(Mwanamke anapewa puto na mwanamume.)
Kujifunza zaidi, tafadhali nenda kwenye ukurasa wa "Mwalimu tufundishe."
Mwalimu Tufundishe
MORAIMASU
Kwanza, kumbuka kuwa AGEMASU inamaanisha "kumpatia mtu kitu," na KUREMASU inamaanisha "mtu anakupatia kitu." Na MORAIMASU inamaanisha “kupokea.”
Tanakali Sauti
Hisia
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kenta alinipa mkufu ulio na umbo la Mlima Fuji. Uligusa sana moyo wangu na nikaanza kuhisi JÎN.