Somo la 44
Baada ya kula vitamutamu vya Kijapani, unakunywa chai ya kijani.

Baada ya kutembelea kasri la Himeji, Anna amehudhuria hafla ya chai kwenye nyumba iliyo karibu ambapo hafla hiyo hufanyika.
Usemi wa msingi:
WAGASHI O TABETE KARA, MACCHA O NOMIMASU.
Mazungumzo
アンナ | 和菓子はとても甘いですね。 | Vitamutamu vya Kijapani ni vitamu sana, au siyo?
|
---|---|---|
Anna | WAGASHI WA TOTEMO AMAI DESU NE.
Vitamutamu vya Kijapani ni vitamu sana, au siyo?
|
|
先生 | 和菓子を食べてから、抹茶を飲みます。 抹茶は苦いかもしれません。 |
Baada ya kula vitamutamu vya Kijapani, unakunywa chai ya kijani. Chai hiyo inaweza kuwa chungu. |
Mwalimu | WAGASHI O TABETE KARA, MACCHA O NOMIMASU. MACCHA WA NIGAI KAMOSHIREMASEN. Baada ya kula vitamutamu vya Kijapani, unakunywa chai ya kijani.
Chai hiyo inaweza kuwa chungu.
|
|
アンナ | 先生、足がしびれました。いたたたた。 | Mwalimu, miguu yangu imekufa ganzi.
Ah, ah, ah, uui!
|
Anna | SENSEI, ASHI GA SHIBIREMASHITA. ITATATATA.
Mwalimu, miguu yangu imekufa ganzi.
Ah, ah, ah, uui!
|
Vidokezo vya sarufi
KAMOSHIREMASEN
KAMOSHIREMASEN inaamisha "inaweza kuwa."
k.m.) NIGAI KAMOSHIREMASEN. (Inaweza kuwa chungu.)
Mwalimu Tufundishe
Umbo la TE la kitenzi + KARA
Katika somo la 16, ulijifunza kwamba unaweza kuelezea zaidi ya tukio moja kwenye sentensi moja kwa kuunganisha vitenzi vya umbo la TE.
Tanakali Sauti
Kufa ganzi
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kuketi huku umekunja miguu yako ni jambo gumu. Nimeelekezwa namna nzuri ya kuzuia miguu isife ganzi. Ni kuketi huku vidole gumba vya miguuni vikiwa pamoja. Wakati mwingine nitajaribu kuketi hivyo.
