NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > MORAIMASU (Somo la 45)

Mwalimu Tufundishe

MORAIMASU (Somo la 45)

Kwanza, kumbuka kuwa AGEMASU inamaanisha "kumpatia mtu kitu," na KUREMASU inamaanisha "mtu anakupatia kitu." Na MORAIMASU inamaanisha “kupokea.”
Kwa Kijapani, unachagua neno utakalotumia kulingana na kiima, kama ni mtoaji au mpokeaji na pia inategemea, mpokeaji ni nani. Ikiwa mtoaji ndiye kiima, unatumia AGEMASU au KUREMASU. 
Ikiwa mpokeaji ni wewe, au mtu mwenye uhusiano wa karibu na wewe, unatumia KUREMASU.

Ikiwa mpokeaji ni wewe mwenyewe, au mtu aliye na uhusiano wa karibu na wewe, unatumia KUREMASU. Kwa mfano, ukitaka kusema “Kenta atanipatia picha”, picha ni SHASHIN. “Mimi” ni WATASHI. Unatumia, NI, kuonyesha mpokeaji. Kwa hiyo, “Kenta atanipatia picha” ni KENTA WA WATASHI NI SHASHIN O KUREMASU.

Ikiwa mpokeaji hana uhusiano wa karibu na wewe, unatumia AGEMASU. Kwa hiyo, "Kenta amempatia Anna picha" itakuwa KENTA WA ANNA NI SHASHIN O AGEMASU.
Ikiwa mpokeaji ndiye kiima, unatumia MORAIMASU (kupewa/kupokea). Tumia NI, kuonyesha mtoaji.
Ikiwa Anna atapewa picha na Kenta, ANNA ni kiima. Mtoaji ni Kenta. Kwa hiyo unasema KENTA NI. “Anna atapewa picha na Kenta” ni ANNA WA KENTA NI SHASHIN O MORAIMASU.

Iwapo utapokea kitu kutoka kwa mkuu wako, itakuwa vyema ukitumia ITADAKIMASU, badala ya MORAIMASU.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.