NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Kuelezea uwezekano (Somo la 41)

Mwalimu Tufundishe

Kuelezea uwezekano (Somo la 41)

Unaweza kuelezea uwezekano, ikiwa utatumia vitenzi vya umbo la kikamusi na kuongeza KOTO GA DEKIMASU (ninaweza kufanya). Tutunge sentensi kutumia usemi KOTO GA DEKIMASU. Unaposema, “ninaweza kwenda,” “mimi” ni WATASHI. “Kwenda” ni IKIMASU. Na umbo lake la kikamusi ni IKU. Hivyo, unaongeza KOTO GA DEKIMASU. Na kusema WATASHI WA IKU KOTO GA DEKIMASU (ninaweza kwenda). Ili kubadilisha sentensi hii iwe katika hali ya kukanusha, unabadilisha DEKIMASU kuwa DEKIMASEN. Kwa hiyo, “siwezi kwenda” ni WATASHI WA IKU KOTO GA DEKIMASEN.
Bila shaka unakumbuka umbo la uwezekano la vitenzi, ulilojifunza katika somo la 35.
Umbo la uwezekano la kitenzi IKIMASU (kwenda) ni IKEMASU (naweza kwenda). Ina maana sawa na IKU KOTO GA DEKIMASU. Lakini IKEMASU ni kauli ya kawaida kuliko IKU KOTO GA DEKIMASU.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.