Somo la 41
Nilifurahi kwa kuwa niliweza kwenda kwenye tamasha la chuoni.
Anna amepona homa. Leo anaandika barua pepe kwa Kenta, ambaye alimtembeza mjini Shizuoka.
Usemi wa msingi:
GAKUEN-SAI NI IKU KOTO GA DEKITE, TANOSHIKATTA DESU
Mazungumzo
アンナ | 健太様 お元気ですか。 |
Ndugu Kenta Hujambo? |
---|---|---|
Anna | KENTA SAMA OGENKI DESU KA. Ndugu Kenta
Hujambo? |
|
アンナ | この間はありがとうございました。 | Asante sana kwa siku ile.
|
Anna | KONOAIDA WA ARIGATÔ GOZAIMASHITA.
Asante sana kwa siku ile.
|
|
アンナ | 学園祭に行くことができて、楽しかったです。 | Nilifurahi kwa kuwa niliweza kwenda kwenye tamasha la chuoni.
|
Anna | GAKUEN-SAI NI IKU KOTO GA DEKITE, TANOSHIKATTA DESU.
Nilifurahi kwa kuwa niliweza kwenda kwenye tamasha la chuoni.
|
|
アンナ | 次は東京で会いましょう。 | Tutakutana Tokyo wakati mwingine.
|
Anna | TSUGI WA TÔKYÔ DE AIMASHÔ.
Tutakutana Tokyo wakati mwingine.
|
Vidokezo vya sarufi
Kitenzi cha umbo la kikamusi + KOTO GA DEKIMASU
Unaweza kuelezea uwezekano, ikiwa utatumia vitenzi vya umbo la kikamusi na kuongeza KOTO GA DEKIMASU (kuweza kufanya_).
Kujifunza zaidi, tafadhali nenda kwenye ukurasa wa "Mwalimu tufundishe."
Mwalimu Tufundishe
Kuelezea uwezekano
Unaweza kuelezea uwezekano, ikiwa utatumia vitenzi vya umbo la kikamusi na kuongeza KOTO GA DEKIMASU (ninaweza kufanya). Tutunge sentensi kutumia usemi KOTO GA DEKIMASU. Unaposema, “ninaweza kwenda,” “mimi” ni WATASHI. “Kwenda” ni IKIMASU. Na umbo lake la kikamusi ni IKU. Hivyo, unaongeza KOTO GA DEKIMASU. Na kusema WATASHI WA IKU KOTO GA DEKIMASU (ninaweza kwenda).
Tanakali Sauti
Kwisha kwa uchovu au wasiwasi
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Nilimuandikia bibi yake Sakura barua badala ya barua pepe. Kiutamaduni, lugha ya Kijapani unatakiwa kuandika kwa wima, kutoka kulia kwenda kushoto. Halikuwa jambo rahisi. Nitamuomba Sakura anihakikie.