NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Kivumishi + SÔ (Somo la 17)

Mwalimu Tufundishe

Kivumishi + SÔ (Somo la 17)

OMOSHIROSÔ, ni "Inaonekana kuvutia."
Ikiwa utaongeza SÔ baada ya kivumishi, unaweza kuzungumzia kile ambacho unakifikiria au unabahatisha baada ya kuangalia au kusikiliza kuhusu kitu fulani.

Katika somo la 13, ulifahamishwa ya kwamba kuna aina mbili ya vivumishi kwa Kijapani. Moja ni aina ya vivumishi vya I ambavyo vinaishia na I, kama vile OMOSHIROI (kuvutia) na ISOGASHII (kuwa na shughuli nyingi). Aina nyingine ya kivumishi ni NA. NA huongezwa baada ya vivumishi hivyo ikiwa vitajitokeza kabla ya nomino. HIMA (Huru au kutokuwa na shughuli) ni miongoni mwao.

Ikiwa utaweka SÔ, usemi unaotumika wakati unapobahatisha, baada ya kivumishi cha I, unabadilisha I kuwa SÔ.
Kwa mfano, ISOGASHII (kuwa na shughuli nyingi), inageuka na kuwa ISOGASHISÔ (unaonekana kuwa na shughuli nyingi).

Kwa vivumishi vya NA, unaongeza SÔ peke yake kwenye vivumishi hivyo. Kwa mfano, HIMA (kutokuwa na shughuli) inageuka na kuwa HIMASÔ (unaonekana kutokuwa na shughuli).
Sasa, utajifunza namna ya kubadilisha SÔ iwe katika hali ya kukanusha. Katika upande wa vivumishi vya I, unabadilisha I na kuwa KU NASASÔ. Kwa mfano, ISOGASHII (kuwa na shughuli nyingi) inageuka na kuwa ISOGASHIKU NASASÔ (unaonekana kutokuwa na shughuli nyingi).

Kwa vivumishi vya NA, unaweka DEWA NASASÔ baada ya vivumishi. Kwa mfano, HIMA (kutokuwa na shughuli)inageuka na kuwa, HIMA DEWA NASASÔ (Unaonekana una shughuli).
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.