Somo la 32
Napenda zaidi futoni.

Anna atalala katika nyumba ya bibi yake Sakura. Hii ni mara yake ya kwanza kulala kwenye futoni, ambalo ni godoro la kijapani na matandiko yake.
Usemi wa msingi:
FUTON NO HÔ GA SUKI DESU
Mazungumzo
さくら | 布団とベッドとどちらが好き? | Unapenda kulala kwenye futoni au kitandani?
|
---|---|---|
Sakura | FUTON TO BEDDO TO DOCHIRA GA SUKI?
Unapenda kulala kwenye futoni au kitandani?
|
|
アンナ | 布団のほうが好きです。 この布団はベッドよりやわらかいです。 |
Napenda zaidi futoni. Futoni hili ni laini kuliko godoro linalowekwa kitandani. |
Anna | FUTON NO HÔ GA SUKI DESU. KONO FUTON WA BEDDO YORI YAWARAKAI DESU. Napenda zaidi futoni.
Futoni hili ni laini kuliko godoro linalowekwa kitandani.
|
|
アンナ | それじゃ、おやすみなさい。 | Basi, usiku mwema.
|
Anna | SOREJA, OYASUMINASAI.
Basi, usiku mwema.
|
|
さくら | おやすみ。 | Nawe pia usiku mwema.
|
Sakura | OYASUMI.
Nawe pia usiku mwema.
|
Vidokezo vya sarufi
A TO B TO DOCHIRA GA Kivumishi DESU KA
Unapomtaka mtu alinganishe sifa za A na zile za B, unasema A TO B TO DOCHIRA GA na baada ya hapo unataja kivumishi kikifuatiwa na DESU KA.
k.m.)
FUTON TO BEDDO TO DOCHIRA GA SUKI DESU KA. (Unapenda kulala kwenye futoni au kitandani?)
Mwalimu Tufundishe
Kauli ya kulinganisha kwa kutumia NO HÔ GA na YORI
Vivumishi vya Kijapani havina mnyambuliko wa ulinganifu. Kwa hiyo, unaelezea ulinganifu kwa kutumia YORI (kuliko), na NO HÔ GA (zaidi).
Tanakali Sauti
Ulaini
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kwa mara ya kwanza nimelala kwenye futoni. Bibi alikuwa amelianika juani kwa ajili yangu. Kwa hiyo, lilikuwa FUKA FUKA na lenye starehe.
