NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Umbo la wakati uliopita la vivumishi (Somo la 19)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la wakati uliopita la vivumishi (Somo la 19)

Umejifunza ya kwamba kuna aina mbili ya vivumishi kwa Kijapani, yaani vya aina ya I na NA. Vivumishi vya I ni vile ambavyo vinaishia na silabi I, kama vile "rahisi" YASUI. Vivumishi vya NA ni vile ambavyo vinaweka NA mwishoni mwake ili kuvumisha nomino. Mfano ni “kupenda,” SUKI,. Inapovumisha nomino, inageuka na kuwa SUKINA. Kwa hiyo, kitabu cha manga unachokipenda, unasema SUKINA MANGA. Ili upate wakati uliopita wa kivumishi cha I, unabadilisha I na kuwa KATTA. Kwa mfano, umbo la wakati uliopita la YASUI, (bei rahisi), ni YASUKATTA. Umbo la wakati uliopita la TAKAI (ghali) ni TAKAKATTA.
Lakini neno ambalo peke yake halifuatii kanuni hiyo ni YOKATTA (ilikuwa vizuri) ambalo umejifunza katika somo hili. Linanyambulika katika hali ambayo si ya kawaida. Umbo la wakati uliopo wa neno hilo ni II (nzuri), ambalo linageuka na kuwa YOKATTA katika umbo la wakati uliopita. Kwa hiyo kitu cha msingi ni kukumbuka hilo.

Ili ubadilishe vivumishi vya I ili viwe katika umbo la kukanusha la wakati uliopita, unabadilisha I na kuwa KU NAKATTA. Kwa mfano, YASUI (bei rahisi) inabadilika na kuwa YASUKU NAKATTA, (haikuwa bei rahisi). II (nzuri) inabadilika na kuwa YOKU NAKATTA (haikuwa nzuri),
Ili vivumishi vya NA viwe katika umbo la wakati uliopita, unaongeza DATTA mwisho wa kivumishi. Kwa hiyo, SUKI (kupenda) inabadilika na kuwa SUKI DATTA (nililipenda). BENRI (kufaa) inageuka na kuwa BENRI DATTA (ilifaa).

Ili ubadilishe vivumishi vya NA viwe katika umbo la kakunusha na wakati uliopita, unaongeza DEWA NAKATTA. SUKI (kupenda), inageuka na kuwa SUKI DEWA NAKATTA (sikupenda).
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.