NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 16

Somo la 16

Tafadhali panda ngazi, na uelekee upande wa kulia.

Anna amefika kwenye duka la kuuza vitabu ambalo liko Shinjuku pamoja na rafiki zake. Anna anamwuliza muuzaji upande ulio na katuni za manga.

Somo la 16 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

KAIDAN O AGATTE, MIGI NI ITTE KUDASAI

Mazungumzo

店員 いらっしゃいませ。 Karibuni.
Muuzaji IRASSHAIMASE.
Karibuni.
アンナ あのう、マンガ売り場はどこですか。 Samahani, katuni za manga ziko upande gani?
Anna ANÔ, MANGA URIBA WA DOKO DESU KA.
Samahani, katuni za manga ziko upande gani?
店員 2階です。階段を上がって、右に行ってください。 Ghorofa ya pili. Tafadhali panda ngazi, na uelekee upande wa kulia.
Muuzaji NIKAI DESU. KAIDAN O AGATTE, MIGI NI ITTE KUDASAI.
Ghorofa ya pili. Tafadhali panda ngazi, na uelekee upande wa kulia.

Vidokezo vya sarufi

Vitenzi vya umbo la TE vinaweza kuunganisha sentensi

Kwa kutumia umbo la TE, unaweza kuelezea vitendo vinavyotokea kwa kufuatana.
k.m.)
KAIDAN O AGARIMASU. (Kupanda ngazi.)
+ MIGI NI ITTE KUDASAI. (Tafadhali uelekee upande wa kulia.)
= KAIDAN O AGATTE, MIGI NI ITTE KUDASAI. (Tafadhali panda ngazi, na uelekee upande wa kulia.)

Mwalimu Tufundishe

Jinsi ya kutumia NI
Ikiwa kitenzi kinaonyesha uwepo, kama IMASU (kuwepo), NI inaonyesha pale ambapo kitu fulani kipo. Kwa mfano, "niko stesheni" ni WATASHI WA EKI NI IMASU.

Tanakali Sauti

TONTON
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Wauzaji kwenye maduka nchini Japani ni wakarimu. Pia ni waungwana kulingana na namna wanavyozungumza. Wanasema "Asante sana" hata kama utaondoka bila kununua kitu chochote.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.