NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Namna ya kuuliza maswali (Somo la 2)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kuuliza maswali (Somo la 2)

Unapouliza maswali kwa Kijapani, hubadilishi mpangilo wa maneno. Unachofanya ni kuongeza kitamkwa, KA mwisho wa sentensi na kusema kwa toni ya juu.
Kwa hiyo, KORE WA OMIYAGE DESU (Hii ni zawadi), ukitaka iwe swali, inakuwa KORE WA OMIYAGE DESU KA (Je hii ni zawadi?)

Sasa, tutafautishe tena sentensi ya kawaida na ile ya swali.

KORE WA OMIYAGE DESU. (Hii ni zawadi.)
KORE WA OMIYAGE DESU KA. (Je hii ni zawadi?) Na ikiwa haufahamu ni kitu gani kilichoko mbele yako, na unataka kuuliza ni kitu gani, unasema KORE WA NAN DESU KA. (Hii ni nini?)
Pia unaweza kutumia NAN (nini), kuuliza muda kwa kuongeza JI (wakati) kwenye neno hilo. Kwa hiyo unasema NAN JI DESU KA. (Ni saa ngapi?) Pia, unaweza kuuliza ni watu wangapi kwa kusema NAN pamoja na NIN, ambayo inamaanisha idadi ya watu, na useme NAN NIN DESU KA. (Kuna watu wangapi?)
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.