Somo la 2
Hii ni nini?

Anna, mwanafunzi kutoka Thailand, alijitambulisha kwa Sakura, mwelekezi wake. Anna anampa Sakura kitu.
Usemi wa msingi:
KORE WA NAN DESU KA
Mazungumzo
アンナ | さくらさん。はい、どうぞ。 | Sakura. Hii ni kwa ajili yako.
|
---|---|---|
Anna | SAKURA-SAN. HAI, DÔZO.
Sakura. Hii ni kwa ajili yako.
|
|
さくら | これは何ですか。 | Hii ni nini?
|
Sakura | KORE WA NAN DESU KA.
Hii ni nini?
|
|
アンナ | それはタイのお土産です。 | Hiyo ni zawadi kutoka Thailand.
|
Anna | SORE WA TAI NO OMIYAGE DESU.
Hiyo ni zawadi kutoka Thailand.
|
|
さくら | ありがとうございます。 | Asante sana.
|
Sakura | ARIGATÔ GOZAIMASU.
Asante sana.
|
|
アンナ | どういたしまして。 | Karibu.
|
Anna | DÔITASHIMASHITE.
Karibu.
|
Vidokezo vya sarufi
A NO B
NO inaunganisha nomino mbili. Katika Kijapani, nomino A inavumisha nomino B.
k.m.) TOKYO NO OMIYAGE (zawadi kutoka Tokyo)
Mwalimu Tufundishe
Namna ya kuuliza maswali
Unapouliza maswali kwa Kijapani, hubadilishi mpangilo wa maneno. Unachofanya ni kuongeza kitamkwa, KA mwisho wa sentensi na kusema kwa toni ya juu.
Tanakali Sauti
Kutembea
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Ndoto ya Sakura ni kufundisha lugha ya Kijapani nje ya nchi. Ndoto yangu ni kusoma katuni za manga kwa Kijapani. Ni kusoma, kusoma, kusoma na mimi!
