NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Misamiati na Majaribio > Orodha ya Misamiati

Orodha ya Misamiati na Majaribio

Somo la 7

すみません [SUMIMASEN]

Samahani
Neno hilo hutumika kumuomba mtu akusikilize. Ikiwa umepotea njia, unaweza kusema SUMIMASEN kwa mpita njia na ukamuuliza muelekeo. Lakini pia unaweza kutumia SUMIMASEN ikiwa unataka kuomba radhi.

Maneno na semi katika somo

アンナ ケーキがいっぱいありますね。 Kuna keki nyingi.
Anna KÊKI GA IPPAI ARIMASU NE.
Kuna keki nyingi.
さくら すみません、シュークリームはありますか。 Samahani, kuna skonzi za krimu?
Sakura SUMIMASEN, SHÛKURÎMU WA ARIMASU KA.
Samahani, kuna skonzi za krimu?
店員 はい、こちらです。 Ndiyo, upande huu.
Muuzaji HAI, KOCHIRA DESU.
Ndiyo, upande huu.
さくら シュークリームを2つください。 Skonzi mbili za krimu, tafadhali.
Sakura SHÛKURÎMU O FUTATSU KUDASAI.
Skonzi mbili za krimu, tafadhali.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.