NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 5

Somo la 5

Hizo ni hazina zangu.

Anna amemwalika Sakura kwenye chumba chake bwenini. Sakura aliona kitu.

Somo la 5 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

SORE WA WATASHI NO TAKARAMONO DESU

Mazungumzo

アンナ 私の部屋はこちらです。どうぞ。 Chumba changu kiko upande huu. Karibu.
Anna WATASHI NO HEYA WA KOCHIRA DESU. DÔZO.
Chumba changu kiko upande huu. Karibu.
さくら すごい!これは全部マンガ? Inashangaza! Zote hizi ni katuni za manga?
Sakura SUGOI! KORE WA ZENBU MANGA?
Inashangaza! Zote hizi ni katuni za manga?
アンナ それは私の宝物です。
私は毎日マンガを読みます。
Hizo ni hazina zangu.
Mimi huwa ninasoma katuni za manga kila siku.
Anna SORE WA WATASHI NO TAKARAMONO DESU.
WATASHI WA MAINICHI MANGA O YOMIMASU.
Hizo ni hazina zangu.
Mimi huwa ninasoma katuni za manga kila siku.

Vidokezo vya sarufi

Kiima WA Mtendwa O Kitenzi

Mpangilio wa maneno kwa Kijapani ni "kiima, mtendwa, na  kitenzi."
O inaonyesha mtendwa.
k.m.) WATASHI WA MANGA O YOMIMASU. (Ninasoma manga.)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kuweka kitenzi katika hali ya kukanusha na swali
Vitenzi vinavyoisha na MASU vinaitwa “vitenzi vya umbo la MASU.” Utatumia umbo la MASU, ikiwa unazungumza kiungwana. Ili tuigeuze ilete dhana ya kukanusha, tunageuza MASU iwe MASEN. Kwa hiyo, YOMIMASU (kusoma) inabadilika na kuwa YOMIMASEN.

Tanakali Sauti

Kusoma vitabu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Pengine Sakura alifikiria mimi huwa ninasoma katuni za manga kila wakati bila kufanya jambo jingine. Lakini kwangu mimi, Manga ni nyenzo nzuri za kujifunza Kijapani.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.