NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Namna ya kuweka kitenzi katika hali ya kukanusha na swali (Somo la 5)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kuweka kitenzi katika hali ya kukanusha na swali (Somo la 5)

Vitenzi vinavyoisha na MASU vinaitwa “vitenzi vya umbo la MASU.” Utatumia umbo la MASU, ikiwa unazungumza kiungwana. Ili tuigeuze ilete dhana ya kukanusha, tunageuza MASU iwe MASEN. Kwa hiyo, YOMIMASU (kusoma) inabadilika na kuwa YOMIMASEN. Ili igeuke na kuwa swali, tunaongeza KA mwisho wa sentensi, na kuisema kwa toni ya juu. Swali linalotokana na YOMIMASU (kusoma) ni YOMIMASU KA.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.