NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Jinsi ya kutumia NI (Somo la 16)

Mwalimu Tufundishe

Jinsi ya kutumia NI (Somo la 16)

Ikiwa kitenzi kinaonyesha uwepo, kama IMASU (kuwepo), NI inaonyesha pale ambapo kitu fulani kipo. Kwa mfano, "niko stesheni" ni WATASHI WA EKI NI IMASU.

Ikiwa kitenzi kinaonyesha mwenendo au mabadiliko kama vile IKIMASU (kwenda), NI inaonyesha mwisho wa mwenendo husika. Kwa mfano, "ninakwenda kwenye kituo cha treni" ni WATASHI WA EKI NI IKIMASU.

NI pia inaonyesha muda maalum, kama vile tarehe au saa.
Kwa mfano, ikiwa utasema "Anna atakuja saa nne," kwa Kijapani, saa nne ni JÛJI, "kuja" ni KIMASU. Kwa hiyo unasema ANNA WA JÛJI NI KIMASU. Hata hivyo, huwezi kutumia NI pamoja na maneno kama vile kesho au juma lijalo, kwa sababu tarehe huenda zikabadilika, ikitegemea na wakati unapozungumza.
Kwa hiyo, ikiwa unataka kusema “Anna atakuja kesho,” "kesho" ni ASHITA. Kwa hiyo, unasema ANNA WA ASHITA KIMASU. Huwezi kusema ANNA WA ASHITA NI KIMASU.

NI pia inaweza kutumika kwa namna mbalimbali.
Tutajifunza kadiri zitakavyojitokeza.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.