NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Namna ya kuboresha Kijapani chako (Somo la 48)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kuboresha Kijapani chako (Somo la 48)

Umekuwa ukijifunza mambo ya msingi katika lugha ya Kijapani kwa mwaka mmoja.

Kama unavyofahamu ni kwamba, ukiongea Kijapani unatakiwa kuchagua namna ya kuongea yaani kiungwana au kawaida, kutegemea na uhusiano wako na msikilizaji. Kwenye masomo yote, Anna aliongea kiungwana, alipozungumza na wakuu wake yaani mwalimu, mama msimamizi wa bweni na Sakura ambaye ni mwelekezi wake. Hata hivyo, alipokuwa akizungumza na Rodrigo, ambaye ni mwanafunzi mwenzake, mwanzoni alitumia kauli za kiungwana kwa kuweka neno DESU au MASU mwishoni mwa sentensi, lakini baadaye wakawa marafiki na kuanza kuzungumza naye kwa namna ya kawaida.

Lugha ni namna ya mawasiliano. Hata kama unafahamu sarufi kwa ufasaha, uhusiano wako na wengine unaweza kuzorota, ikiwa utashindwa kuzungumza kwa namna inayoendana na hali husika. Kwa upande mwingine, hata kama utafanya makosa ya kisarufi, tumaini lako la kuwa na uhusiano mzuri na wengine linaweza kuwasilishwa, ikiwa utajaribu kutumia lugha ya kiungwana au ya kawaida katika hali husika.

Hivyo jitahidi kuzungumza Kijapani mara nyingi iwezekanavyo, ili upate uzoefu wa lugha yenyewe katika hali mbalimbali. Hili ndilo jambo la msingi katika kujifunza lugha. Kila la kheri!
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.