Somo la 48
Asante kwa yote
Leo, Anna anarejea nchini Thailand. Sakura na Kenta wamekwenda uwanja wa ndege kumuaga.
Usemi wa msingi:
IROIRO OSEWA NI NARIMASHITA
Mazungumzo
健太 | 体に気をつけて。 | Nakutakia afya njema.
|
---|---|---|
Kenta | KARADA NI KIOTSUKETE.
Nakutakia afya njema.
|
|
さくら | タイに着いたら連絡してね。 | Ukiwasili nchini Thailand, tafadhali tujulishe.
|
Sakura | TAI NI TSUITARA, RENRAKU SHITE NE.
Ukiwasili nchini Thailand, tafadhali tujulishe.
|
|
アンナ | はい。いろいろお世話になりました。 | Sawa. Asante kwa yote.
|
Anna | HAI. IROIRO OSEWA NI NARIMASHITA.
Sawa. Asante kwa yote.
|
|
アンナ | 健太さんとさくらさんもお元気で。 | Kenta na Sakura, pia nawatakia afya njema.
|
Anna | KENTA-SAN TO SAKURA-SAN MO OGENKIDE.
Kenta na Sakura, pia nawatakia afya njema.
|
Vidokezo vya sarufi
KIOTSUKETE
KIOTSUKETE ni umbo la TE la kitenzi KIOTSUKEMASU (kuwa mwangalifu). Unatumia NI kuonyesha kile unachotakiwa kuwa makini nacho.
k.m.) KURUMA NI KIOTSUKETE.
(Kuwa mwangalifu na magari.)
Mwalimu Tufundishe
Namna ya kuboresha Kijapani chako
Umekuwa ukijifunza mambo ya msingi katika lugha ya Kijapani kwa mwaka mmoja.
Tanakali Sauti
Kicheko
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kila mmoja, SAYÔNARA (kwa heri), hadi tutakapokutana tena. Nitakapokuja Japani wakati mwingine, nitakuwa ninazungumza Kijapani kwa ufasaha zaidi. U FU FU!