NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Umbo la amri la vitenzi (Somo la 25)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la amri la vitenzi (Somo la 25)

Hivi ndiyo jinsi ya kutengeneza umbo la amri kutoka kitenzi cha umbo la MASU. Kwanza, kwa vitenzi vinavyomalizia na irabu "E" kwenye silabi kabla tu ya MASU, unabadilisha MASU na kuwa RO. Kwa mfano, “kula,” TABEMASU, inabadilika na kuwa TABERO, (Kula!). Kuna namna mbili za kubadilisha vitenzi vinavyoishia na irabu "I" kwenye silabi za kabla ya MASU.
Namna ya kwanza ni kubadilisha MASU na kuwa RO. “Kuamka” yaani OKIMASU inabadilika na kuwa OKIRO (Amka!).

Namna ya pili, unaondoa neno MASU na kubadilisha irabu kwenye silabi kabla tu ya MASU na kuwa "E." “Kuingia”, HAIRIMASU, kitenzi kinachotumika katika usemi wa leo, kinanyambulika hivi. Kinakuwa HAIRE, (Ingia!).

Lakini neno pekee ambalo halifuati kanuni hii ni “kuja,” yaani KIMASU. Linageuka na kuwa KOI (Njoo!).
Umbo la amri la vitenzi linaashiria ulazimishaji wa jambo fulani.
Mara nyingi linatumiwa na mwanamume, anapomuambia rafiki yake wa karibu au mtoto afanye kitu fulani. Wanawake hawatumii usemi huu.

Namna ya kiungwana ya kuamuru inayotumika na wanawake na wanaume, unaweza kuondoa MASU iliyopo kwenye kitenzi cha umbo la MASU na kusema NASAI badala yake.
“Kula,” TABEMASU, inabadilika na kuwa TABENASAI. Na “kuingia,” HAIRIMASU, inabadilika na kuwa HAIRINASAI.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.