Somo la 25
Ingia chini ya dawati.

Anna amehudhuria darasa la somo la Kijapani na jengo la shule likaanza kutikisika.
Usemi wa msingi:
TSUKUE NO SHITA NI HAIRE
Mazungumzo
先生 | 地震だ。みんな、落ち着いて。 机の下に入れ。 |
Ni tetemeko. Nyote, muwe watulivu. Ingia chini ya dawati.
|
---|---|---|
Mwalimu | JISHIN DA. MINNA, OCHITSUITE. TSUKUE NO SHITA NI HAIRE. Ni tetemeko. Nyote, muwe watulivu. Ingia chini ya dawati.
|
|
先生 | 揺れは収まったようだ。 | Inaonekana mitetemo imetulia.
|
Mwalimu | YURE WA OSAMATTA YÔ DA.
Inaonekana mitetemo imetulia.
|
|
アンナ | びっくりした。日本は本当に地震が多いですね。 | Nilishangazwa. Kwa kweli Japani hushuhudia mitetemo mingi, au siyo?
|
Anna | BIKKURI SHITA. NIHON WA HONTÔ NI JISHIN GA ÔI DESU NE.
Nilishangazwa. Kwa kweli Japani hushuhudia mitetemo mingi, au siyo?
|
Vidokezo vya sarufi
YÔ DA / YÔ DESU
YÔ DA ni namna ya kawaida ya YÔ DESU, inayoonyesha kwamba mzungumzaji ametathmini hali ilivyo na kufanya maamuzi fulani kuhusiana na hali hiyo.
Kabla ya YÔ DA, huwezi kutumia vitenzi vya umbo la MASU.
k.m.) YURE WA OSAMATTA YÔ DA.
(Inaonekana mitetemio imekwisha.)
* OSAMATTA = Umbo la TA la OSAMARIMASU (kutulia)
Tofauti kati ya WA na GA
WA: inaonyesha mada
GA: inaonyesha kiima
WA inaonyesha mada ya sentensi. Na kiima kina uhusiano na mada, na kinaonyeshwa na GA na wakati mwingine WA.
k.m.) ZÔ WA HANA GA NAGAI.
(Kuhusu ndovu, mikonga yao ni mirefu.)
Mwalimu Tufundishe
Umbo la amri la vitenzi
Hivi ndiyo jinsi ya kutengeneza umbo la amri kutoka kitenzi cha umbo la MASU. Kwanza, kwa vitenzi vinavyomalizia na irabu "E" kwenye silabi kabla tu ya MASU, unabadilisha MASU na kuwa RO. Kwa mfano, “kula,” TABEMASU, inabadilika na kuwa TABERO, (Kula!).
Tanakali Sauti
Kutikisika
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Tetemeko la ardhi linapotokea, kitu cha kwanza unachohitajika kufanya ni kupata taarifa kupitia redio au runinga. Niliambiwa nifanye hivyo.
