NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Aina mbili za vivumishi (Somo la 13)

Mwalimu Tufundishe

Aina mbili za vivumishi (Somo la 13)

Kuna vivumishi vya aina mbili. Vile vinavyomalizikia na silabi I, na vile ambavyo havimalizikii na silabi hiyo. Vile vinavyomalizikia na silabi I vinaitwa vivumishi vya I. Vinajumuisha HIROI (pana), na ATARASHII (mpya).

Vivumishi vinawekwa kabla ya nomino. Kwa mfano “kitabu kipya" ni ATARASHII HON. Kwa vivumishi ambavyo havimalizikii na silabi I, unaongeza NA iwapo utavitumia kama vivumishi kabla ya nomino. Kwa hiyo vinaitwa vivumishi vya NA. Mfano ni SUKI neno ambalo lipo katika mazungumzo yetu ya leo, yaani kupenda. Unaweza kufikiria ni kivumishi cha I. Lakini huo siyo ukweli. Kinaishia na silabi ya KI. Kwa hiyo, “kitabu ninachopenda” inakuwa SUKINA HON.
Lakini kuna baadhi ya maneno ambayo hayatumii kigezo hicho. Baadhi ya vivumishi vya NA vinamalizikia na silabi ya I. Maneno hayo ni pamoja na KIREI (nzuri au safi), YÛMEI (maarufu), na TOKUI (hodari). Kwa hiyo, “kitabu kizuri” siyo KIREI HON, bali ni KIREINA HON.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.