NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Namna ya kutumia "Jifunze Kijapani"

Namna ya kutumia "Jifunze Kijapani"

Katika "Jifunze Kijapani", kwa wale wanaoanza, wanaweza kujifunza Kijapani kupitia jumla ya masomo 48. Ufuatao ni mfano wa namna ya kujifunza kwenye tovuti hii.

1.
Msingi wa mafunzo ni sauti iliyo kwenye kila somo. Kwanza bofya kitufe cha kucheza sauti kilicho na namba ya somo 1 katika kila ukurasa na sikiliza somo zima. Katika muda wa dakika 10, unaweza kujifunza maana ya usemi na sarufi katika kila somo. Maelezo kuhusu sarufi ni ya muhimu zaidi, hivyo sikiliza mara kadhaa hadi uelewe.
2.
Bofya kitufe cha "Kusikiliza zote" 2 kwenye sehemu ya maandishi, sikiliza mazungumzo yote mara kadhaa. Ikiwa utabofya kwenye michoro 3, unaweza kusikiliza sauti hiyohiyo pamoja na michoro ya wahusika.
3.
Bofya kitufe chenye alama ya kipaza sauti pembezoni mwa sentensi 4 kwenye sehemu ya maandishi, fanya mazoezi ya kuzungumza wakati ukisikiliza, huku ukijaribu kuiga jinsi wahusika wanavyozungumza. Anza kwa kufuatisha sehemu zile tu ambazo unaweza kuiga, lakini pia fanya mazoezi kwa kuzungumza namna hiyo mara kadhaa.
4.
Ukizoea, fanya mazoezi ukifuatilia mazungumzo yote. Jaribu kutamka mara baada ya sauti. Ni muhimu kuanza kutamka kabla ya kuishia sauti.

Baadae, ukipitia tena sehemu zinazofuata, itakusaidia kuongeza uelewa wako.

Mazungumzo Mazungumzo
[Mazungumzo] 5
Haya ni maandishi yote, sauti na tafsiri ya somo zima. Inakuwezesha kusikiliza sauti ya somo zima, na pia kusikiliza kila sentensi. Tafadhali sikiliza mara kadhaa na ujaribu kukumbuka misemo hiyo. Sehemu hii inakuwezesha kuongeza uelewa na matamshi yako pia.
Vidokezo vya sarufi
[Vidokezo vya sarufi] 6
Maelezo ya kisarufi yaliyojumuishwa kwenye sauti ya somo, yamefupishwa kwenye sehemu hii.
Mwalimu Tufundishe
[Mwalimu Tufundishe] 7
Msimamizi wa masomo haya Profesa Akane Tokunaga, anaelezea mambo muhimu katika somo linalofundishwa.
[Tanakali Sauti] 8
Tanakali sauti zinaelezwa kwa sauti na michoro.
[Herufi za Kijapani] 9
Herufi za Kijapani za "Hiragana" na "Katakana" nazo zinatambulishwa.
[Orodha ya Misamiati na Majaribio] 10
Maneno na misemo ya msingi iliyotumika kwenye somo nayo yanatambulishwa. Pia kuna jaribio la kuthibitisha kuwa umeelewa maana.
[Tafakuri ya Anna] 11
Mhusika mkuu Anna anaelezea tafakuri yake jinsi anavyohisi, na kile alichojifunza kwa kuishi nchini Japani.