#4
Kusema unachotarajia kufanya
Tam anazungumza na rafiki yake mpya, Mi Ya, mpigapicha kutoka China. Chumba cha Mi Ya kimepambwa kwa picha nyingi kutoka kote nchini Japani.
へえ。
Hee.
Wow!
これ
kore
hii
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
どこ
doko
wapi
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
沖縄
Okinawa
Okinawa
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
へえ
hee
wow
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
京都
Kyooto
Kyoto
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
とても
totemo
sana
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
きれい(な)
kiree (na)
‐zuri / pendeza
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
そうですね
soo desu ne
Hakika
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
日本
Nihon
Japani
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
何
nani
nini
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
する
suru
fanya
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
大学
daigaku
chuo kikuu
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
日本語
Nihongo
lugha ya Kijapani
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
勉強する
benkyoo-suru
jifunza / soma
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
いい
ii
‐zuri
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
はい
hai
ndio
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
楽しみ(な)
tanoshimi (na)
tazamia
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
Kusema unachotarajia kufanya
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
Ili kuelezea utakachofanya, tumia kitenzi cha umbo la MASU (chenye kuishia na neno "masu") kama vile "benkyoo-shimasu" yaani "nitasoma." Umbo hilo hutumika unapozungumza kiungwana. "De" ni kiunganishi kinachoashiria mahali na "o" ni kiunganishi kinachoelezea shamirisho. Kitenzi huja mwishoni mwa sentensi.
Makundi ya vitenzi na unyambulishaji:
*Umbo la msingi la vitenzi kama "kau" yaani "kununua," "taberu" yaani "kula," na "benkyoo-suru" yaani "kujifunza," huitwa umbo la kikamusi (ambapo vitenzi huorodheshwa kwenye kamusi).
*Vitenzi vimegawanyika katika makundi matatu kulingana na namna vinavyonyambulika.
Vitenzi katika kundi la kwanza vinavyoishia na "-u," sehemu ya "-u" hunyambulika.
Vinaweza kugawanywa kama hivi "kau (ka + u)" yaani "kununua," "nomu (nom + u) " yaani "kunywa," na "iku (ik + u) " yaani "kwenda."
Vitenzi katika kundi la pili vinavyoishia na "-ru", "-ru" hunyambulika. Vitenzi hivyo vinaweza kugawanywa kama hivi "miru (mi + ru)" yaani "kutazama," na "taberu (tabe + ru)" yaani "kula."
Vitenzi katika kundi la tatu ni vile vinavyobadilika kwa kutofuata kanuni za kunyambulika. Kundi hili lina vitenzi viwili tu: "kuru" yaani "kuja." na "suru/~suru." yaani "kufanya."
Tazama jedwali la mnyambuliko kwa mengi zaidi.
*Ili kutengeneza umbo la MASU kutokana na vitenzi vya kwenye umbo la kikamusi katika kundi la kwanza, badili "-u" iishie na "i" na kisha ongeza "masu" ("ka+u→ka+i masu").
Katika vitenzi vya kundi la pili, badili "-ru" iwe "-masu" ("tabe + ru→tabe + masu").
Vitenzi katika kundi la tatu (vitenzi visivyofuata kanuni za kunyambulika) vinanyambulika kama hivi: "kuru→kimasu" na "suru→shimasu."
Umbo la MASU la vitenzi hutumika kuelezea si tu utakachofanya bali pia kitendo cha mazoea na masuala ya jumla.
Jifunze zaidi
1Chaguo lipi kati ya machaguo haya matatu ni namna sahihi ya kusema sentensi hii kwa lugha ya Kijapani?
Nitakula tempura.
tempura | kula
天ぷら | 食べます(食べる)
tenpura | tabemasu (taberu)
2Sema sentensi hii kwa lugha ya Kijapani, ukitumia neno/maneno yafuatayo.
Nita~ [shamirisho].
【shamirisho】 を~ます。
【shamirisho】 o~masu.
Kabuki | tazama
歌舞伎 | 見ます(見る)
kabuki | mimasu (miru)
3Sema sentensi hii kwa lugha ya Kijapani, ukitumia neno/maneno yafuatayo.
Nita~ [shamirisho].
【shamirisho】 を~ます。
【shamirisho】 o~masu.
zawadi | nunua
お土産 | 買います(買う)
omiyage | kaimasu (kau)
Ongeza kwenye "kumbukumbu zangu"Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
Huu ni usemi unaoelezea kitu unachokitarajia kwa furaha.
Mwongozo wa safari wa Mi Ya
Uzuri wa sehemu mbalimbali nchini Japani
Unaweza kufurahia mandhari ya misimu minne tofauti kote nchini Japani. Kwa mfano, msimu wa machipuo ni msimu wa kuchanua kwa maua ya micheri. Kyoto iliyotajwa kwenye somo hili ni sehemu maarufu kwa maua hayo. Katika msimu wa joto, watu wengi hufurahia kupanda milima na kwenda kwenye fukwe. Katika msimu wa pukutizi, kubadilika kwa rangi ya majani kunapendeza sana. Na msimu wa baridi pia unavutia kwa sababu ya theluji. Unaweza kufurahia kuteleza kwenye theluji na michezo mingine ya baridi.
(1) Hokkaido
(2) Nikko, Mkoa wa Tochigi
(3) Kyoto
(4) Okinawa
Imeongezwa kwenye "kumbukumbu zangu"
Tayari ipo kwenye "kumbukumbu zangu"