Jinsi ya kutumia tovuti hii

Katika "Jifunze Kijapani", kwa wale wanaoanza, wanaweza kujifunza Kijapani kupitia jumla ya masomo 48. Ufuatao ni mfano wa namna ya kujifunza kwenye tovuti hii.

Somo

Msingi wa mafunzo ni sauti iliyo kwenye kila somo. Kwanza bofya kitufe cha kucheza sauti kilicho na namba ya somo 1 katika kila ukurasa na sikiliza somo zima. Katika muda wa dakika 10, unaweza kujifunza maana ya usemi na sarufi katika kila somo. Maelezo ya usemi wa msingi ni ya muhimu zaidi, hivyo sikiliza mara kadhaa hadi uelewe.

Bofya kitufe cha picha jongevu 2, sikiliza mazungumzo yote mara kadhaa. Unaweza kuchagua tafsiri ya mazungumzo 3, kama vile Kiswahili, Kijapani, na hakuna.

Bofya kitufe chenye alama ya kipaza sauti pembezoni mwa sentensi 4 kwenye sehemu ya mazungumzo, fanya mazoezi ya kuzungumza wakati ukisikiliza, huku ukijaribu kuiga jinsi wahusika wanavyozungumza. Anza kwa kufanyia mazoezi semi za msingi na semi za ziada.

Ukitaka kujifunza zaidi, fanya mapitio kwenye sehemu zifuatazo. Itakusaidia kuimarisha uelewa wako.


Mazungumzo

Haya ni maandishi yote na tafsiri zake kutoka kwenye mazungumzo ya somo. Unaweza kusikiliza sauti ya sentensi hadi sentensi. 5 Tafadhali sikiliza kwa kurudia na kumbuka semi hizo. Kipengele hiki kinakusaidia kuboresha ufahamu pamoja na matamshi.

Matamshi yameelezewa katika alfabeti za kirumi. 6

Sauti zinazotamkwa kwa kuvuta zimeelezewa kwa kurudia sauti ya irabu (mf. "tokee" yaani saa). Na unatakiwa kuweka pozi kabla ya kutamka konsonanti ambayo itakuwa imeandikwa kwa kurudiwa mara mbili (mf. "zasshi" yaani jarida).


Msamiati

Maneno na semi zilizotumika kwenye mazungumzo zimeorodheshwa hapa. Bofya "Ongeza kwenye kumbukumbu zangu" 7 na hifadhi vyote unavyotaka kukumbuka katika Kumbukumbu Zangu.

Unaweza kutafuta maneno na semi. 8


Usemi wa Msingi

Lengo la somo. (Can-do) 9

Maelezo kuhusu matumizi na sarufi ya usemi wa msingi ambao ni muhimu ili kufikia Can-do. 10

Bofya "Ongeza kwenye Kumbukumbu zangu" 11 na hifadhi semi za msingi unazotaka kukumbuka katika Kumbukumbu Zangu.


Tumia!

Mifano ya mazungumzo, inayotumia semi za msingi. Sikiliza sauti 12 na zirudie.


Jaribu!

Mazoezi. Unda sentensi kwa kutumia maneno yaliyooneshwa.


Usemi wa ziada

Semi za kwenye mazungumzo ambazo unaweza kuzitumia kwa kuwa zipo kwenye mazungumzo ya kila siku. Hifadhi semi unazotaka kuzikumbuka katika Kumbukumbu Zangu. 13

Sikiliza sauti 14 ili kufahamu jinsi usemi unavyotumika katika mazungumo ya kila siku.


Ongeza maarifa

Jifunze salamu, jinsi ya kuhesabu namba, siku za juma na semi zingine zenye manufaa.


Kanji

Utambulishaji wa Kanji, herufi za kiideografia zinazotumika Japani.


Utamaduni

Taarifa kuhusu utalii, utamaduni, chakula, maadili na mambo mengine kuhusiana na somo husika.


Haru-san wangu

Ukurasa huu ni mahususi kwa ajili yako.

Hifadhi maendeleo yako kwenye "Niliyokwisha jifunza." 15

Unapata kibanio cha nywele cha Haru-san 16 kila wakati unapotembelea "somo" au "tumia!"

Unapata 〇 17 kila unapopata jibu sahihi katika "Jaribu!"

Unaweza kuhifadhi kwenye "Kumbukumbu zangu" semi unazotaka kukumbuka kutoka kwenye semi za msingi, semi za ziada, maneno na misamiati. 18

Tengeneza kumbukumbu zako za misamiati.


Pakua (sauti/maandishi)

Unaweza kupakua sauti katika MP3 na maandishi katika PDF bure.

Kupakua kumewekewa ukomo kwa matumizi binafsi.


Herufi za Kijapani

Herufi za Kijapani za Hiragana, Katakana na Kanji zipo. Unaweza kupakua majedwali ya herufi za Hiragana na Katakana.