Herufi za Kijapani
Lugha ya Kijapani ina aina tatu ya herufi: Hiragana, Katakana na Kanji. Hiragana na Katakana ni herufi za fonetiki, kila moja ikiwakilisha silabi moja. Jifunze herufi za Kijapani kama hatua ya mwanzo ya kujifundisha kusoma na kuandika Kijapani.
Bofya ili uhakikishe matamshi!
Herufi za Kijapani unazoweza kuzipakua
Baada ya kupakua orodha ya herufi za Hiragana na Katakana na kuzichapisha kwenye karatasi, unaweza kufanya mazoezi ya kuziandika kwa kuzifuatisha juu ya herufi hizo. Tunaeleza pia namna ya kuandika hatua kwa hatua. Hiyo ni hatua muhimu ya kuandika herufi za Kijapani vizuri.