NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Faida za kujifunza Kijapani kupitia NHK WORLD

Faida za kujifunza Kijapani kupitia NHK WORLD

Faida za kujifunza Kijapani kupitia NHK WORLD

Jifunze Kijapani kupitia NHK WORLD!!

Faida 6 muhimu za kujifunza!!

Anza Kujifunza Kijapani sasa hivi kwenye mtandao bure!

Tuseme kwamba ndiyo umeamua kujifunza lugha ya Kijapani, lakini huwezi kwenda shule au kusikiliza redio kwa muda huo kila siku.

Kwa kutumia Jifunze Kijapani ya NHK WORLD, unaweza kujifunza namna ya kuzungumza Kijapani kwa urahisi.

Jifunze Kijapani kupitia NHK WORLD, inaweza kufanyika kwenye mtandao wakati wowote wa siku na bure. Unachotakiwa kufanya ni kubonyeza kwenye somo unalotaka kujifunza na kuanza kusikiliza. Anza sasa kujifunza namna ya kuzungumza Kijapani kwenye mtandao bure.

Masomo mbalimbali yanaanza kwa mambo ya msingi!
Ni rahisi kwa watoto kujifunza pia

Tuna masomo katika viwango mbalimbali, hivyo usiwe na wasiwasi hata kama ndiyo kwanza unaanza. Watu ambao ndiyo wameanza kujifunza Kijapani wanaweza kuanza kwa mambo ya msingi na kuimarisha uwezo wao kutoka hapo. Masomo pia ni mazuri kwa wale wanaotaka kuimarisha uwezo wao wa kusikiliza na kuzungumza.

Kwa wazazi ambao wanataka watoto wao waanze masomo ya lugha ya Kijapani, NHK WORLD ni njia muafaka. Masomo ni mafupi, hivyo watoto hawatachoka. Fanya mazoezi nyumbani na watoto wako! Chagua mbinu bora ya kujifunza inayokufaa.

Jifunze vizuri kwa kutumia faili za sauti za Wajapani

Kama hauko Japani, ni vigumu kupata shule yenye walimu wenye asili ya Kijapani.

Kwanza wakati unajifunza lugha mpya, ni muhimu kusikiliza matamshi ya wazungumzaji asilia na kufanya mazoezi kwa kuigiza jinsi wanavyozungumza. Fikiria kuwa uko Japani kwa mapumziko na unataka kumuuliza mtu kituo cha treni kilipo. Unajua jinsi ya kusema, lakini mara unapojaribu kumuuliza mtu, hawezi kukuelewa. Hata kama unajua semi, huwezi kuzitumia kwenye hali halisi.

Kuepuka hili, ni vyema ukajifunza matamshi na lafudhi kutoka kwa wazawa wa Japani.

Njia rahisi na ya haraka kujifunza

Kwa watu wenye kazi nyingi na hawawezi kusikiliza redio kwa muda huo kila siku, au ambao hawana muda wa kwenda shuleni kila wiki, huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kukosa kipindi cha NHK WORLD.

Masomo yote kwenye sauti na maandishi yanapatikana kwenye tovuti ya Jifunze Kijapani ya NHK WORLD. Hivyo unaweza kujifunza Kijapani kupitia vipindi vyetu wakati unapojisikia kufanya hivyo. Unaweza pia kusikiliza masomo tena na tena, na hivyo kama huna uhakika kuhusu somo unaweza kurudi nyuma na kusikiliza tena.

Pia huhitaji kusikiliza masomo ambayo tayari unayajua.

Chagua masomo unayotaka kutoka kwenye orodha ya masomo.

Unaweza kutafuta na kuhifadhi masomo kwa mfumo wa MP3

Kama una kazi nyingi na huna muda wa kusikiliza masomo kwenye kompyuta, tafuta na hifadhi kwa mfumo wa MP3. Unaweza kusikiliza masomo ukiwa njiani kwenda kazini au shuleni. Pia unaweza kusikiliza masomo nyumbani wakati unafua ama unafanya kazi nyingine. Huhitaji kubadilisha ratiba yako ya kujifunza Kijapani kila siku. Tumia muda wako vizuri na anza kujifunza Kijapani na NHK WORLD.

Unaweza hata kutafuta na kuhifadhi maandishi kwa mfumo wa PDF

Kama unatafuta na kuhifadhi faili ya PDF, unaweza kuona maudhui ya masomo yote mara moja. Ukiyachapisha, unaweza kutengeneza kitabu na kukibeba popote unapotaka.

Kupitia NHK WORLD unaweza kujifunza kwenye mtandao wakati wowote bure.

Unachotakiwa kufanya ni kubonyeza somo unalotaka kujifunza na kuanza kusikiliza.

Anza sasa kujifunza namna ya kuzungumza Kijapani kwenye mtandao bure.