NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Misamiati na Majaribio > Orodha ya Misamiati

Orodha ya Misamiati na Majaribio

Somo la 7

ふたつ [FUTATSU]

vipande viwili
Inajumuisha “mbili” na TSU, ambayo ni kiambishi cha kuhesabu vitu kama vile keki. Ikifuatana na TSU, namna ya kuhesabu namba moja hadi kumi hubadilika.
Tafadhali nenda kwenye "Nyenzo za kujifunzia."

Maneno na semi katika somo

アンナ ケーキがいっぱいありますね。 Kuna keki nyingi.
Anna KÊKI GA IPPAI ARIMASU NE.
Kuna keki nyingi.
さくら すみません、シュークリームはありますか。 Samahani, kuna skonzi za krimu?
Sakura SUMIMASEN, SHÛKURÎMU WA ARIMASU KA.
Samahani, kuna skonzi za krimu?
店員 はい、こちらです。 Ndiyo, upande huu.
Muuzaji HAI, KOCHIRA DESU.
Ndiyo, upande huu.
さくら シュークリームを2つください。 Skonzi mbili za krimu, tafadhali.
Sakura SHÛKURÎMU O FUTATSU KUDASAI.
Skonzi mbili za krimu, tafadhali.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.