NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Misamiati na Majaribio > Orodha ya Misamiati

Orodha ya Misamiati na Majaribio

Somo la 47

1周 [ISSHÛ]

mzunguko mmoja
Inajumuisha namba, ICHI (moja), na kiambishi cha kuhesabu SHÛ (mzunguko). Lakini unasema ISSHÛ, badala ya ICHISHÛ.

Maneno na semi katika somo

先生 最後に、みなさんの夢を教えてください。 Mwisho, tafadhali tuelezeeni ndoto zenu.
Mwalimu SAIGO NI, MINASAN NO YUME O OSHIETE KUDASAI.
Mwisho, tafadhali tuelezeeni ndoto zenu.
ロドリゴ 僕は日本を1周したいです。 Nataka kutembelea kote nchini Japani.
Rodrigo BOKU WA NIHON O ISSHÛ SHITAI DESU.
Nataka kutembelea kote nchini Japani.
アンナ 私は…日本語教師になるのが夢です。 Kwa upande wangu... ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani.
Anna WATASHI WA... NIHONGO-KYÔSHI NI NARU NO GA YUME DESU.
Kwa upande wangu... ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.