NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Misamiati na Majaribio > Orodha ya Misamiati

Orodha ya Misamiati na Majaribio

Somo la 45

お誕生日おめでとう [OTANJÔBI OMEDETÔ]

Kheri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa!
OTANJÔBI ni usemi wa kiungwana ikiwa na TANJÔBI (siku ya kuzaliwa) ambayo inajumuisha O kabla yake. Ikiwa unataka kusema kwa kauli ya kiungwana zaidi unaweza kusema OTANJÔBI OMEDETÔ, na kuongeza GOZAIMASU baada yake.

Maneno na semi katika somo

みんな アンナ、お誕生日おめでとう。 Anna, heri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa!
Wote ANNA, OTANJÔBI OMEDETÔ.
Anna, heri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa!
健太 これ、ほんの気持ちです。 Hiki ni kitu kidogo kwa ajili yako.
Kenta KORE, HONNO KIMOCHI DESU.
Hiki ni kitu kidogo kwa ajili yako.
アンナ どうもありがとうございます。 Nakushukuru sana.
Anna DÔMO ARIGATÔ GOZAIMASU.
Nakushukuru sana.
さくら 何をもらったの? Umepewa nini?
Sakura NANI O MORATTA NO?
Umepewa nini?
アンナ 開けてもいいですか。 Ninaweza kufungua?
Anna AKETE MO II DESU KA.
Ninaweza kufungua?
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.