NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Misamiati na Majaribio > Orodha ya Misamiati

Orodha ya Misamiati na Majaribio

Somo la 2

さん [SAN]

Bwana, Bibi, au Bi
Unapomuita mtu kwa jina lake Kijapani, unaongeza neno SAN baada ya jina kuonesha heshima.
Vilevile unaweza kusema CHAN baada ya jina la msichana mdogo na KUN baada ya jina la mvulana mdogo. Maneno haya kwa kawaida huongezwa mbele ya majina ya watoto wadogo kabla ya kujiunga na shule ya msingi.

Maneno na semi katika somo

アンナ さくらさん。はい、どうぞ。 Sakura. Hii ni kwa ajili yako.
Anna SAKURA-SAN. HAI, DÔZO.
Sakura. Hii ni kwa ajili yako.
さくら これは何ですか。 Hii ni nini?
Sakura KORE WA NAN DESU KA.
Hii ni nini?
アンナ それはタイのお土産です。 Hiyo ni zawadi kutoka Thailand.
Anna SORE WA TAI NO OMIYAGE DESU.
Hiyo ni zawadi kutoka Thailand.
さくら ありがとうございます。 Asante sana.
Sakura ARIGATÔ GOZAIMASU.
Asante sana.
アンナ どういたしまして。 Karibu.
Anna DÔITASHIMASHITE.
Karibu.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.