NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Misamiati na Majaribio > Orodha ya Misamiati

Orodha ya Misamiati na Majaribio

Somo la 1

よろしくお願いします [YOROSHIKU ONEGAI SHIMASU]

Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa.
Unapojitambulisha kwa mtu unasema YOROSHIKU ONEGAI SHIMASU. Katika muktadha huu ikimaanisha, "Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa." Pia unaweza kutumia usemi huo kama ishara ya kukamilisha mazungumzo wakati ambapo unamuomba mtu akufanyie jambo fulani.

Maneno na semi katika somo

アンナ はじめまして。私はアンナです。 Nashukuru kukutana nawe.
Mimi ni Anna.
Anna HAJIMEMASHITE.
WATASHI WA ANNA DESU.
Nashukuru kukutana nawe. Mimi ni Anna.
さくら はじめまして。さくらです。 Nami pia.
Mimi ni Sakura.
Sakura HAJIMEMASHITE.
SAKURA DESU.
Nami pia. Mimi ni Sakura.
アンナ よろしくお願いします。 Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa.
Anna YOROSHIKU ONEGAI SHIMASU.
Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa.
さくら こちらこそ。 Ni mimi ninayestahili kusema hivyo.
Sakura KOCHIRAKOSO.
Ni mimi ninayestahili kusema hivyo.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.