NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Vitenzi vya umbo la TE - Namna mbalimbali (Somo la 9)

Mwalimu Tufundishe

Vitenzi vya umbo la TE - Namna mbalimbali (Somo la 9)

Katika somo lililotangulia ulijifunza namna rahisi ya kubadilisha kitenzi cha umbo la MASU iwe kitenzi cha umbo la TE. Unachofanya ni kubadilisha MASU iwe TE.

Leo, tujifunze namna nyingine ya kutengeneza umbo la TE. Katika mtindo huu, haubadilishi MASU peke yake bali pia silabi moja kabla ya MASU. Ikiwa silabi iliyopo kabla ya neno MASU ni RI, unabadilisha RI na MASU pamoja, yaani RIMASU, kuwa TTE.
Kwa hiyo, ATSUMARIMASU (kukusanyika), inakuwa ATSUMATTE. Kanuni hii pia inatumika, ikiwa silabi kabla ya MASU ni I au CHI. Hapa, pia unabadilisha I au CHI pamoja na MASU na kuwa TTE.

Ikiwa silabi kabla ya MASU ni MI, NI au BI, unabadilisha silabi hiyo pamoja na MASU kuwa NDE. Kwa mfano, YOMIMASU (Kusoma) inakuwa YONDE.

Sasa, Ikiwa silabi kabla ya MASU ni KI, unaweza kubadilisha silabi hiyo na MASU kwa pamoja kuwa ITE. Kwa hiyo, KIKIMASU (Kusikiliza) inakuwa KIITE. Ikiwa silabi kabla ya MASU ni GI, unabadilisha silabi hiyo na MASU kwa pamoja kuwa IDE. Kwa hiyo, ISOGIMASU (kufanya haraka) inakuwa ISOIDE.

IKIMASU (kwenda) ndiyo neno pekee ambalo halizingatii kanuni hiyo. Linabadilika na kuwa ITTE. 

Tukariri hilo kwa kuimba. Wimbo huu unakufahamisha vile unavyoweza kubadilisha vitenzi vya umbo la MASU hadi umbo la TE, ikitegemea na silabi zinazojitokeza kabla ya MASU.

Tafadhali angalia ukurasa wa "Nyenzo za kujifunzia."
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.