NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Kitenzi cha umbo la TE + KUDASAI (Somo la 8)

Mwalimu Tufundishe

Kitenzi cha umbo la TE + KUDASAI (Somo la 8)

Kwa Kijapani unapomuomba mtu afanye kitu, unasema kwa kutumia vitenzi vya umbo la TE, kisha unaongeza KUDASAI (Tafadhali). Vitenzi vya umbo la TE ni vile vinavyonyambulika ambavyo vinaishia na TE au DE.

Kwa Mfano, unataka kuwaomba wengine wakumbuke kitu fulani. Unatumia kitenzi cha umbo la TE cha OBOEMASU (kukumbuka), ambacho ni OBOETE, kisha unaongeza KUDASAI na unazisema kwa pamoja yaani OBOETE KUDASAI. Sasa, nikueleze juu ya namna ya kubadilisha vitenzi vya umbo la MASU kwenda kwenye umbo la TE, kama OBOEMASU, ambayo umbo lake la TE ni OBOETE.

Namna ya msingi ni kubadilisha tu MASU kwenye TE.
Kwa mfano, kitenzi kinachomaanisha “kula” ni TABEMASU. Umbo lake la TE linakuwa TABETE. Kwa hiyo, TABETE KUDASAI inamaanisha “Tafadhali kula.”
“Kuangalia” ni MIMASU. Umbo lake la TE linakuwa MITE.
Kwa hiyo, MITE KUDASAI inamaanisha “Tafadhali angalia.”
“Kufanya” ni SHIMASU. Umbo lake la TE linakuwa SHITE.
Kwa hiyo, SHITE KUDASAI ni “Tafadhali fanya (kitu fulani).”
“Kuja” ni KIMASU. Umbo lake la TE ni KITE. Kwa hiyo, KITE KUDASAI inamaanisha “Njoo tafadhali.”

Unaweza kupata vitenzi vya umbo la TE kwa kubadilisha MASU na kuwa TE. Ni rahisi bila shaka.
Vitenzi vinavyobadilika namna hii vina irabu "E" kwenye silabi zao kabla tu ya MASU. Vinajumuisha OBOEMASU (kukumbuka). Pia vinajumuisha baadhi ya vitenzi ambavyo vina irabu "I" kwenye silabi zao kabla tu ya MASU, kama MIMASU (kuangalia).

Kwenye somo lijalo tutakufahamisha namna nyingine ya kutengeneza vitenzi vya umbo la TE.
Unapoanza kujifunza Kijapani, huenda ukakuta vitenzi vya umbo la TE ni vigumu kuelewa. Lakini tujitahidi kujifunza pamoja.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.