NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Namna ya kutumia kitenzi cha ARIMASU (Somo la 7)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kutumia kitenzi cha ARIMASU (Somo la 7)

ARIMASU (kuna) ni kitenzi kinachoelezea kuwepo kwa vitu. Kiima cha ARIMASU kinaonyeshwa na GA.

Kimsingi, unatumia GA, unapomtambulisha mtu au kitu kwenye mazungumzo kwa mara ya kwanza.
Hiyo ndiyo sababu, Anna alipoingia kwenye duka la kuuza keki, alisema KÊKI GA IPPAI ARIMASU NE (Kuna keki nyingi). Hapa, aliitaja keki kwa mara ya kwanza na kutokana na hilo alitumia GA kuonyesha kiima. Sakura anasema SHÛKURÎMU WA ARIMASUKA (Kuna skonzi za krimu?), kwa kutumia WA ambayo inaonyesha mada.
Hapa, Sakura yuko kwenye duka la kuuza keki na anaangalia kila aina ya keki. Lakini anataka kujua ikiwa miongoni mwa keki zote hizo kuna skonzi ya krimu. Kutokana na hilo anachukua skonzi za krimu kama mada, na kutumia WA inayoonyesha mada.

Mfano mwingine, pengine umekwenda dukani kununua shati, lakini hauoni lililo kubwa la saizi ya L. Wataki huo utamuuliza mhudumu hivi, ERU SAIZU WA ARIMASU KA (Kuna saizi kubwa?).
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.