NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Namna ya kubadilisha vitenzi na kuwa nomino (Somo la 47)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kubadilisha vitenzi na kuwa nomino (Somo la 47)

Ukitaka kubadilisha vitenzi kuwa nomino, unaongeza NO au KOTO kwenye kitenzi cha muundo wa kawaida, kama vile umbo la kikamusi au umbo la TA.

Acha nikuelezee hili kwa kutumia usemi wa msingi kwa hii leo “Ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani.” Ili kubadilisha kitenzi NARIMASU (kuwa) kiwe nomino, unaongeza NO kwenye umbo la kikamusi la NARIMASU, ambalo ni NARU. Na inakuwa NARU NO, ambayo ni nomino, Hivyo basi, “Ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani.” ni NIHONGO-KYÔSHI NI NARU NO GA YUME DESU.

Unaweza kutumia KOTO, badala ya NO. Kwa hiyo, NARU NO (kuwa) pia inaweza kuwa NARU KOTO. Ikiwa utatumia NARU KOTO, sentensi hiyo itabadilika na kuwa, NIHONGO-KYÔSHI NI NARU KOTO GA YUME DESU.

Lakini unaweza tu kutumia KOTO, ikiwa utabadilisha kitenzi kabla tu ya DESU mwisho wa sentensi. Kwa mfano, unaweza kusema sentensi hiyo hiyo "Ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani" kwa kutumia WATASHI NO YUME, yaani "ndoto yangu." WATASHI NO YUME WA NIHONGO-KYÔSHI NI NARU KOTO DESU.
Kwa upande mwingine, unaweza tu kutumia NO kubadilisha vitenzi kuwa nomino, ikiwa vitenzi vinavyoelezea hisia kama vile kusikia au kuona vinakuja baada ya NO.
Tuchambue sentensi ifuatayo, “Ninaweza kusikia ndege wakiimba.”

“Ndege” ni TORI. “Kuimba” ni NAKIMASU. Umbo lake la kikamusi ni NAKU. Kwa hiyo, “Ndege wakiimba” ni TORIGA NAKU NO GA. Kisha, “Naweza kusikia” ni KIKOEMASU. Kwa pamoja, “Ninaweza kusikia ndege wakiimba.” ni TORI GA NAKU NO GA KIKOEMASU.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.