NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Umbo la kikamusi + MAE NI (Somo la 46)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la kikamusi + MAE NI (Somo la 46)

MAE NI (kabla ya) ni kauli ya kusisitiza unachofanya au ulichofanya, kabla ya kufanya kitu kingine. Vitenzi huwa kwenye umbo la kikamusi, ikiwa vitafuatiwa na MAE NI. Hata kama sentensi yote iko katika hali ya wakati uliopita, kitenzi kinachukua umbo la kikamusi kabla ya MAE NI, japo umbo hili linaashiria wakati uliopo.

Je, ukitaka kusema “Kabla ya kula chakula, nilinawa mikono,” unasemaje kwa Kijapani? “Chakula” ni GOHAN. “Kula“ ni TABEMASU. Umbo lake la kikamusi ni TABERU. “Mikono ” ni TE. “Kuosha” ni ARAIMASU, na umbo lake la wakati uliopita ni ARAIMASHITA. Kwa hiyo kwa pamoja unasema GOHAN O TABERU MAE NI, TE O ARAIMASHITA. Kwa upande mwingine, unatumia ATO DE (baada ya), unapotaka kusisitiza kuhusu unachofanya au ulichofanya, baada ya kufanya jambo lingine. Unatumia umbo la TA la kitenzi kabla ya ATO DE.
Msikilizaji kama unavyojua umbo la TA la kitenzi linatumika katika kuonyesha wakati uliopita au wakati timilifu. Hata hivyo hapa, hata kama sentensi yote iko katika wakati uliopo, unatumia umbo la TA la kitenzi kabla ya ATO DE.

Na je, ukitaka kusema “Baada ya kula chakula, naosha sahani,” kwa Kijapani unasemaje? Umbo la TA la kitenzi ”kula” ni TABETA. “Sahani” ni SARA. Au kwa namna ya kiungwana, unasema OSARA.
Kwa hiyo kwa ujumla itakuwa GOHAN O TABETA ATO DE, OSARA O ARAIMASU.
Kwa kifupi unatumia vitenzi vya umbo la kikamusi kabla ya MAE NI, na umbo la TA la kitenzi, kabla ya ATO DE. Kumbuka hili kwa pamoja.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.