Mwalimu Tufundishe
Jinsi ya kutengeneza sentensi za kukanusha (Somo la 4)
Tuchukulie mfano huu, "Mimi ni Mjapani.""Mimi" ni WATASHI, na "Mjapani" ni NIHON-JIN.
Kwa hiyo, “Mimi ni Mjapani” ni WATASHI WA NIHON-JIN DESU.
Ili kutengeneza sentensi ya kukanusha kutoka sentensi inayomalizia na DESU, unabadilisha DESU kuwa DEWA ARIMASEN. Kwa hiyo, “Mimi si Mjapani” ni WATASHI WA NIHON-JIN DEWA ARIMASEN. Kwenye sentensi hii, ikiwa utabadilisha DEWA iwe JA, sentensi inageuka na kuwa NIHONJIN JA ARIMASEN. Hii inakuwa ni mazungumzo ya kawaida.