NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Umbo la NAI la kitenzi + NAKEREBA NARIMASEN (Somo la 36)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la NAI la kitenzi + NAKEREBA NARIMASEN (Somo la 36)

Unaposema ni lazima au unahitajika kufanya jambo fulani, unabadilisha sehemu ya NAI katika kitenzi cha umbo la NAI na kuwa NAKEREBA NARIMASEN.

Kwa mfano, ikiwa unataka kusema “Ninapaswa kusoma,” kwanza unabadilisha kitenzi cha BENKYÔ SHIMASU (kusoma) katika umbo la NAI, na kuwa BENKYÔ SHINAI. Kisha unabadilisha NAI kwa kuweka NAKEREBA NARIMASEN. Kwa hiyo unasema, BENKYÔ SHINAKEREBA NARIMASEN. Katika namna ya kawaida, NAKEREBA NARIMASEN, (napaswa), inabadilika na kuwa NAKYA. Kwa hiyo, unasema BENKYÔ SHINAKYA.

Ikiwa huhitajiki kufanya kitu fulani, unabadilisha sehemu ya NAI na kuwa NAKUTEMO II DESU. Kwa hiyo, unaposema “Sina haja ya kusoma,” unabadilisha sehemu ya NAI ya BENKYÔ SHINAI (sitasoma) na kuwa NAKUTEMO II DESU, kisha useme BENKYÔ SHINAKUTEMO II DESU.

Lakini! nimfahamishe kila mmoja ya kwamba ni muhimu kusoma.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.