NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Namna ya kutengeneza vivumishi vya umbo la TE. (Somo la 34)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kutengeneza vivumishi vya umbo la TE. (Somo la 34)

Ikiwa unataka kuelezea kitu kwa kutumia vivumishi viwili au zaidi, unabadilisha kivumishi ama vivumishi vya awali kwenda kwenye umbo la TE.
Sasa, acha nikufundishe namna ya kubadilisha vivumishi kwenye umbo la TE.

Umejifunza kwamba kuna aina mbili ya vivumishi, vile vya I na NA.

Vivumishi vya I ni vile vinavyoishia na silabi "I", kama vile YASUI (bei rahisi).

Kubadilisha kivumishi cha I katika umbo la TE, unabadilisha I ya mwisho wa neno na kuwa KUTE. “Bei rahisi,” yaani YASUI, inabadilika na kuwa YASUKUTE. TANOSHII (kufurahi) inabadilika na kuwa TANOSHIKUTE. Neno la kipekee lisilofuata kanuni hii ni II (nzuri) ambalo linabadilika na kuwa YOKUTE. Vivumishi vya NA huchukua NA mwishoni, vinapovumisha nomino, kama vile GENKI (kuwa na afya). Kwa hiyo, “mtu mwenye afya”, “mtu” ni HITO, hivyo useme GENKINA HITO.

Hata hivyo, kubadilisha vivumishi vya NA katika umbo la TE, unaongeza DE mwishoni mwake. GENKI inabadilika na kuwa GENKIDE.

Ikiwa unataka kusema, “Mtu mwenye afya na mchangamfu,” “mchangamfu” ni AKARUI. Kwa hiyo unasema, GENKIDE AKARUI HITO.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.