NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > O na GO zinazoonyesha heshima (Somo la 31)

Mwalimu Tufundishe

O na GO zinazoonyesha heshima (Somo la 31)

Unapotaka kuonyesha heshima kwa msikilizaji au mtu unayemzungumzia, unasema O au GO kabla ya nomino au vivumishi kuhusiana na mtu huyo. Kwa mfano, SHIGOTO (kazi) inakuwa OSHIGOTO. GENKI (kuwa na afya) inakuwa OGENKI. Na KAZOKU (familia) inakuwa GOKAZOKU. Pia, unapotaka kuzungumza kiungwana, mara nyingi utaongeza O au GO kabla ya nomino. Baadhi ya nomino hujumuishwa na O au GO hata katika mazungumzo ya kawaida. Mfano ni OCHA (chai) na OBÂSAN (bibi) kama ulivyojifunza katika somo hili.

Kwa upande mwingine, baadhi ya nomino huwa haziendani na O wala GO. Hii ni pamoja na maneno yaliyokopwa kutoka lugha za kigeni kama vile KAMERA.

Bila shaka unaweza kujiuliza ni wakati gani unaostahili kutumia O na GO. Unatumia GO mbele ya nomino ambazo asili yake ni China. Kwa nomino nyingine zote, unatumia O. Lakini ni vigumu kutambua ni maneno gani yaliyotoka China. Kwa hiyo, tafadhali kumbuka hayo wakati unapoona nomino zilizo na O au GO.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.