NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > N DA: kauli unayoitumia kuelezea kitu fulani (Somo la 29)

Mwalimu Tufundishe

N DA: kauli unayoitumia kuelezea kitu fulani (Somo la 29)

Umbo la msingi la N DA ni NO DA. Unasema
NO DA mwisho wa sentensi, ikiwa unataka kuelezea kile kinachotokea, sababu au kwa hali gani. Katika mazungumzo ya kawaida, unasema N DA. Kwa namna ya kiungwana unasema N DESU.

Huwezi kutumia vitenzi vya umbo la MASU kabla ya NO DA. Unahitajika kutumia muundo wa kawaida, kama vile umbo la kikamusi au umbo la TA. Kwa hiyo, ukitaka kueleza “mvua itanyesha,” ikiwa wingu kama hilo litaonekana, utasemaje? “Mvua itanyesha” ni AME GA FURIMASU. Unabadilisha FURIMASU (Kunyesha) katika umbo la kikamusi, FURU, na uongoze N DA. Unasema, AME GA FURU N DA. Kwa namna ya kiungwana unasema AME GA FURU N DESU.

NO DA inabadilika na kuwa NANO DA, ikiwa nomino au vivumishi vya NA vinakuja kabla ya NO DA. Katika hali kama hiyo, N DA inabadilika na kuwa NAN DA. Kwa hiyo, ikiwa “kazi,” SHIGOTO, ni sababu, unasema SHIGOTO NAN DA. Kwa namna ya kiungwana, unasema SHIGOTO NAN DESU.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.