NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Kitenzi cha umbo la NAI + DE KUDASAI (Somo la 24)

Mwalimu Tufundishe

Kitenzi cha umbo la NAI + DE KUDASAI (Somo la 24)

Ikiwa unataka kuwaambia wengine kile ambacho hawaruhusiwi kufanya, unajumuisha vitenzi vya umbo la NAI na DE KUDASAI, na useme NAI DE KUDASAI (Tafadhali usifanye hivyo).

Kwa mfano, unasema “Tafadhali usiende.” Umbo la NAI la kitenzi IKIMASU (kwenda) ni IKANAI. Unaongeza DE KUDASAI katika neno hilo na kusema IKANAI DE KUDASAI (tafadhali usiende). Pia kuna misemo inayotumika kuhimiza wengine wasifanye kitu fulani. Katika somo la 22, umejifunza ya kwamba unaweza kutumia kitenzi cha umbo la TE na kuongeza
WA IKEMASEN, kisha useme TE WA IKEMASEN (usifanye hivyo).
Kwa mfano, “Usiende” ni ITTE WA IKEMASEN.

TE WA IKEMASEN inatumiwa ikiwa mkuu anamkaripia mdogo wake au wazazi wanapowafundisha watoto wasifanye jambo fulani.

Wajapani hukwepa kuwapatia wengine msongo wa mawazo. Kwa hiyo mara nyingi husema NAI DE KUDASAI katika mazungumzo yao, badala ya TE WA IKEMASEN.
Usemi mwingine unaosisitiza mtu asifanye jambo fulani ni DAME DESU (Huruhusiwi), kama ulivyousikia katika mazungumzo ya somo la leo.

Kuna namna moja nzuri ya kukataa kitu au jambo ambalo mwingine amekuomba ufanye bila kukera mwingine.
Unasema SORE WA CHOTTO..., (Hiyo, mimi kidogo aah....). Jaribu kuutumia.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.