NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Vivumishi vya umbo la kukanusha (Somo la 15)

Mwalimu Tufundishe

Vivumishi vya umbo la kukanusha (Somo la 15)

Katika somo la 13, tulijifunza ya kwamba kuna aina mbili za vivumishi vya Kijapani, vivumishi vya I na vivumishi vya NA.
Vivumishi vya I vinamalizia na silabi ya I, kama vile ATARASHII (mpya). Na vivumishi vya NA huwa na NA kabla ya nomino. DAIJÔBU (sawasawa), ambalo tumejifunza katika somo hili, ni kivumishi cha NA, ambacho kinageuka na kuwa DAIJÔBUNA kabla ya nomino. Ili ubadilishe kivumishi cha I kiwe katika hali ya kukanusha, unabadilisha I iwe KUNAI. Kwa hiyo, kukanusha kwa ATARASHII (mpya) ni ATARASHIKUNAI (sio mpya).
Kuweka vivumishi vya NA katika hali ya kukanusha, unaongeza DEWANAI. Kwa hiyo, kukanusha kwa DAIJÔBU (sawasawa) ni DAIJÔBUDEWANAI (sio sawa).

Utasikika kawaida, ikiwa utabadilisha DEWANAI iwe JANAI, na useme DAIJÔBUJANAI.

Tafadhali nenda kwenye "Nyenzo za kujifunzia."
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.